SERIKALI YAHITAJIKA KUPUNGUZA UTEGEMEZI

NA NOEL STEPHEN MPWAPWA

 Imebainishwa kuwa serikali bado haiko makini katika  kulifikia lengo la sita la mileniamu katika swala zima la kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu na Ukimwi kwa kuendelea kutegemea misaada kutoka serikali ya watu wa kimarekani.

 Hayo yameibuliwa na wajumbe wa mkutano   wa kamati ya kuratibu shughuli za huduma shirikishi za kifua kikuu na  na ukimwi Wilayani mpwapwa mkoani Dodoma kwenye kikao  cha kutadhimini  huduma hizo hapa  wilayani kilicho fanyika katika ukumbi wa Afya  jana.

Akieleza mmmoja wa wajumbe  alisema katika  TANZANIA lazima itambue kuwa umakini wa utawala bora na uwajibikaji ni kutekeleza malengo waliyo jiwekea  au waliyo iridhia katika mikataba mbalimbali ya kimataifa  ikiwemo kutekeleza  malengo ya  mileniamu  likiwepo  lengo la sita la kupambana  na kifua kikukuu, UKIMWI, na Malaria ili kuweza  kuimarisha maisha bora na utawishaji wa jamii.


Aidha alidai kuwa “haiwezekani  tunapo karibia kumaliza au kufikia mwisho wa  muda  wa malengo ya  mileniamu bado SERIKALI YA Tanzania  inategemea fedha za kuendesha  mipango  shirikishi ya kifua kikuu na ukimwi  inategemea  ufadhili wa  mfuko  wa maendeleo ya  wamarekan(Glob fund) bila serikali yetu kuweka mikakati ya kuweza kulikabili tatizo hili kama ni tatizo la watanzania na walishughulikie wao wenyewe kwa kulitengea bajeti katika  mipango yao ya halmashauri ya ili kuweza kuondoa hali ya utegemezi wa moja kwa moja  kutoka kwa nchi wahisani”.

Akiongea mwenyekiti wa kikao hicho  kaimu mganga mkuu wa wilaya  DR.Pathan Mohamed alisema kuwa   ni vyema halmashauri zetu   kuingiza mpango huu kwenye  bajeti za halimashauri ili kuweza  kulimudu tatizo hili na kulitokemeza kabisa ifikapo  2015 kama maliengo ya mileniamu  yanavyo taka.

Akitoa taarifa  utekekelezaji  mratibu wa shughuli za  huduma za kifua kikuu na UKIMWI  Dr  JASTINI  NYONI alisema kuwa  kuanzia januari 2011-Desemba 2011 aliweza kupima wagojwa  wa kifua kikuu  wapatao wagojwa 191 wakiwemo wanaume 135 na wanawake 56, na walipima  virusi vya UKIMWI  walikuwa wanawake 55 na wanaume 125, ambapo walio kutwa na Virusi vya Ukimwi  ni watu 79 wakiwemo wanawake25 na wanaume 54 amabapo alisema kuwa sawa na asilimia 30% ya wagonjwa walio sajiliwa kwa mwaka jana.

Pia Dr Nyoni alisema kuwa kwa mwaka  2012 wamepokea fedha zipatazo milioni33,895,231/= amabazo zitatumika katika kutoa huduma za upimaji wa makohozi katika vituo vya fya vinavyo toa huduma hii kwa sasa  ili waweze kuboresha huduma hizo.

Tena wadau hao waliweza kutoa wito kwa wana siasa kuto ingilia kazi za kiutendaji ili kuweza kuleta tija katika  huduma shirikishi za mapambano dhidi ya  ukimwi na kifua kikuu kwa kuacha tabia ya kuwakataza wagonjwa kuto changia mfuko wa afya wa wilaya.(CHF)

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.