Posts

Showing posts from June, 2018

LUFU WAPATA BARABARA TANGU UHURU.

Image
SERIKALI wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma   imewataka wakazi wa kata za Mwanawota na Lufu   waliopatiwa fedha za ukarabati   wa barabara kuthaminisha ukabarabati wa barabara hizo   sambamba na uboereshaji uchumi wa kata zao kwa kufanya kazi kwa Bidii. Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa   Jabir Shekimweri alipotembelea   barabara hizo kwa ajili ya kuangalia hali halisi ya ukarabati unaoendelea   katika kata hizo chiniya wakala wa barabara Vijijini TARURA Wilaya ya Mpwapwa. Barabara zilipatiwa fedha za ukarabati   ni barabara ya kibakwe ,Mwanawota yenye urefu wa kilometa 16 yenye dhamani ya shilingi shilingi milion 713,000,000/= na barabara ya kata ya Rufu yenye urefu   wa kilometa   kilometa 16 pia Shekimweri alisema   hakuna zaidi kwa kata hizi kutoa shukrani kwa serikali   ya awamu ya tano zaidi ya kupandisha kiwango cha uchumi katika kata zao   ambazo zimepatiwa fedha za ukarabati. “Haiwezekani barabara zinapendeza zinanga’aa lakini bado uchumi u

UHARIBIFU WA MAZINGIRA WATISHIA JAGWA.

Image
  Baadhi ya akina mama wakipanda mti katika kata ya Mazae KUFUTIA uharibifu mkubwa wa mazingira   unaofanywa na watu katika   wilaya ya   Mpwapwa   kunatishia   kupungua kwa   upatikanaji wa   huduma ya maji   kwa baadhi ya vijiji vya wilaya ya Mpwapwa. Hali hiyo imetanabaishwa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri kwenye   kilele cha siku ya   mazingira   duniani iliyofanyika katika kijiji cha Idilo kata ya Mazae. Shekimweli amesema   uhai na ustawi wa wa   Taifa letu unategemea   sana   mazingira   yanayotuzungunguka   hivyo alisema uharibifu wa mazingira   ni moja   kati   ya tishio   kubwa la uhai wa binadamu na viumbe vingine   vinavyo tegemea mazibgira   katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Aidha Shekimweri amesema   mabadiliko ya   ya tabia   ya nchi   sasa   yamekuwa ni tishio   la usalama   wa mataifa   kama ilivyo   kwa ugaidi na vita . Amesema katika nchi za wenzetu   kama visiwa vya   Maldives ambako   mabadiliko ya   ya nch