ANGETILE AJIONDOA TUME YA UCHAGUZI

nga  Send to a friend
Tuesday, 29 May 2012 21:25
0digg
Jessca Nangawe
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania(TFF), Angetile Osiah amejiondoa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Uchaguzi wa klabu ya Yanga na kusema, uamuzi wake haukusukumwa na taswira ya mgogoro wa uongozi ndani ya klabu hiyo.
Karibu wiki moja iliyopita, Mwenyekiti wa Yanga Llyod Nchunga alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya takribani mwezi mzima wa shinikizo la kumtaka kuchukua uamuzi huo toka kwa wanachama wa klabu hiyo.
Shinikizo la kumtaka Nchunga kuachia nafasi hiyo, kulitanguliwa na  wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo kujiuzulu nafasi zao na kubaki wanne toka 12.
Wakati akijiuzulu, Nchunga alisema amefikia hatua hiyo ili kuepuka kuwa chanzo cha ukosefu wa amani ndani ya Yanga.
Akiongea jana jijini Dar es Salaam, Osiah alisema uamuzi huo umekuwa wa lazima kwa vile siyo rahisi kwake kutumikia kofia mbili kwa wakati mmoja.
"Majukumu yamekuwa mengi, siyo rahisi tena kwangu kutumikia nafasi mbili kwa wakati mmoja, lakini ni vizuri pia nikasisitiza kwamba, uamuzi wangu hauhusiani na kinachoendelea Yanga," alisema Osiah.
Bosi huyo wa TFF alisema, kujiondoa kwake kwenye kamati hiyo ya uchaguzi hakujabeba tafsiri kwamba, hatahusika tena majukumu ya kawaida ndani ya klabu hiyo.
"Nitaendelea kuwa mwanachama halali wa Yanga kwa vile nina kadi iliyo hai. Nitakuwa tayari wakati wowote kushirikiana na uongozi wa Yanga kama watahitaji msaada wangu," alisema Osiah.
Alisema tayari amewasilisha barua ya kujiuzulu nafasi hiyo kwa Katibu mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa.
"Kanuni ya uchaguzi ya Yanga kifungu cha 5 zinaruhusu kujipunguzia majukumu endapo sababu ya kufanya hivyo itakuwapo, hivyo amezingatia na kuheshimu kanuni nikiwa kama mpenda michezo," alisema

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!



7000 symbols left


Banner
Banner

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.