KITUO CHA HAKI ZA BINADAMU WAZIDI KUMTETEA LULU

MAOMBI ya uchunguzi wa umri wa muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na  kesi ya mauaji, yamepangwa kusikilizwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam  Mei 28, 2012.

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hata hivyo, umri wake halali umezua utata kiasijambo ambalo limewalazimu Mawakili wanaomtetea kuwasilisha maombi mahakamani wakiitaka mahakama ifanye uchunguzi wa umri halali wa msanii huyo.

Maombi hayo yaliwasilishwa Mahakama Kuu na mmoja wa mawakili wake, Peter Kibatala, Mei 17.

Habari ambazo Mwananchi lilizipata jana kutoka mahakamani hapo na kuthibitishwa na Wakili Kibatala zinasema kuwa maombi hayo yamepangwa kuanza kusikilizwa Mei 28 na kwamba yamengiwa kusikilizwa na Jaji wa Dk Fauz Twaib.

Katika maombi namba 46 ya mwaka 2012, mawakili hao wanaomtetea msanii huyo wanaiomba Mahakama Kuu itoe uamuzi kama Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kuamua ufanyike uchunguzi wa umri halali wa msanii huyo.
Jopo la mawakili hao maarufu linadai kuwa linaamini kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo kwa sasa ndio bado inayoshughulikia kesi hiyo, ina mamlaka ya kufanya au kuamuru ufanyike uchunguzi wa umri mshtakiwa huyo.

Lakini pia wanaiomba Mahakama Kuu kama itaridhika kuwa Mahakama ya Kisutu haina uwezo huo, basi Mahakama Kuu yenyewe ifanye uchunguzi huo.

Mawakili hao walifikia uamuzi wa kuwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu baada ya maombi ya Mahakama ya Kisutu kujiondoa katika kuyashughulikia.

Akifafanua juu ya maombi hayo Kibatala ambaye pia ni Makamu wa Raisi wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS) alisema kuwa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 kifungu cha 113 inaruhusu Mahakama kufanya uchunguzi wa umri wa mshtakiwa.

Wakili Kibatala alisema lengo la uchunguzi huo ni  ili mahakama iweze kujiridhisha kama mshtakiwa ni mtoto au ni mtu mzima kwa lengo la kujipa angalizo juu ya maslahi ya mtoto.

“Baada ya uchunguzi huo mahakama ikijiridhisha kuwa ni mtoto basi mwenendo wa kesi hiyo utaendeshwa kwa maslahi ya mtoto kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) cha sheria hiyo ya mtoto,” alisema Wakili Kibatala.

Kwa mujibu wa Wakili Kibatala kifungu hich ambacho huelezea ulinzi wa maslahin ya mtoto katika uendeshaji wa kesi kwa watoto wanaokinzana na sheria.
Kabla ya kuwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu, mawakili hao mawakili hao waliwasilisha maombi  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 7,2012  wakiiomba iamuru kesi ya msanii huyo isikilizwe katika mahakama za watoto wakidai kuwa bado ni mtoto.
Mawakili hao walidai mahakamani hapo kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17 na kwamba kwa maana hiyo yeye bado ni mtoto na kesi yake haipaswi kusikilizwa katika mahakama za kawaida kama mtu mzima.
Kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea msanii huyo wakili Kenedy Fungamtama alidai kuwa mteja wao ana umri wa miaka 17 na si 18

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.