Posts

Showing posts from July, 2017

WAIMBAJI WA NYIMBO ZA DINI WAASWA KUFUATA MAADILI.

. WAIMBAJI wa nyimbo za dini Nchini wamekumbushwa kutunga nyimbo za kuhamasisha Amani   na watu kupenda kufanya kazi. Sambamba na hilo   pia waimbaji   wa kike wa   Music wa dini   wametakiwa   wasimame katika uwakili wa kazi ya   Mungu    ya kuomba kwa ajili ya Taifa   na kuombea familia na kubaki katika maadili ya music wao unavyo wataka . Rai hiyo imetolewa jana wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma   na Meneja wa Bank   ya NMB   tawi la Mpwapwa Bi Beatrice Mwasa   katika Uzinduzi   wa   Album ya   mwimbaji wa nyimbo za Dini   Mwalimu   Paulina Ndatila(Mwl Boma) albam inayojulikana kwa jina la TUTATAWALA. Bi Mwasa alisema kumekuwako   na upotovu wa maadili   kwa baadhi ya waimbaji wa nyimbo za dini kwa uvaaji wao ambao hauakisi kile wanacho kiimba Pia alisema waimbaji hao wakitunga nyimbo za njisi ya kupunguza   migogoro   ya familia ambayo inatishia kuongezeka kwa   uvunjifu wa amani   kuanzia ngazi ya familia   hadi taifa . Aidha Bi Mwassa alisema kama akina mama wakisi

WANANCHI WA MLEMBULE WATEMBEA UMBALI WA KILOMETA 40 KUTAFUTA HUDUMA ZA AFYA.

www.facebook.com WANANCHI wa kijiji cha   kijiji cha Mlembule   wilaya   ya Mpwapwa   Mkoa wa Dodoma Huwalazimu   kutembea umbali wa kilometa 12 hadi 40 kufika makao makuu wa wilaya kutafuta huduma za afya kutokana na kijiji   hicho kuto kuwa na kituo cha afya   katika kata hiyo kinachoweza kutoa huduma ya uapasuaji wa dharura kwa akina mama wajawazito. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji hicho   bwana Andason Mwangalimi   alisema   hali   hiyo imekuwa ikiwaathili sana   akina mama   wajawazito    wanapougua   usiku   au ugonjwa wa ghafla. “Kutokana   na hali hii   akina mama huwalazimu kutembea umbali wa kilomita 12 hadi 40    kwasabu kijiji hiki   hakina zahati   na kipindi cha mvua kijiji hiki kinakorongo kubwa lijulikalo kama korongo la manamba   maji yakijaa watu hushidwa kuvuka na kuna mama mjamzito aliwahi kufia hapa   kutokana   na kukosa huduma kwa muda muafak”aliongea   . Bwana Mwangalimi alisema kutokana   na hali   hiyo akina   Mama   wajawazito wamekuwa wakijifung

WANANCHI WATUMIA MTI KAMA CLINIC YA WATOTO.

Image
Wanachi wa kijiji cha Mlembule watumia mti kama clinic ya kupimia watoto.
Image
Wananchi wa NDUGA  kata ya Nduga wakionyeha Mabango juu wA mgogoro Wa  Ardhi katika kijiji hicho. Mkutano ukiendelea katika Mabonde ya mashamba katika kijiji cha Nduga. Diwani wa kata ya Mlembule Wilson Mgunga Akifafanua jambo kwa wanchi wa kata hiyo. Bwana Sudi akitoa utetezi wake kwa wanchi wa kijiji cha Nduga.

DC MPWAPWA AOBWA KUINGILIA KATI MGOGORO WA ARDHI NDUGA.

    WANANCHI wa kijiji cha Nduga kata Mlembule   wilaya ya   Mpwapwa Mkoani Dodoma   wameiomba kamati ya ulinzi na usalama kuingilia kati mgogoro wa mashamba katika bonde la   kijiji hicho unatishia uvunjifu wa amani. Akiongea mmoja wa wananchi wa kijiji hicho na mwenyekiti CCM wa kijiji hicho Tumain Yohana amesema kumewako   hali ya sinto fahamu kutoka   mtu mmoja aliya fahamika kwa jina la Rashid Sudi Makasi      kwa wanachi   kile alicho kisema kuwa kunatishia   wananchi hao kuwafukuza kwa kuwafukuza katika maeneo yao kwa kudai kuwa ni yake. Bwana Tumaini   amesema alisema kuwa kijiji cha nduga kimeanza kulitumia shamba hilo zaidi ya mika arobaini   iliyo pita na ilikuwa moja wapo ya chanzo cha mapato ya kijiji hicho ambapo wanannchi walikuwa wanakodishwa na kulipa kiasi kidogo kwa kijiji na sasa shmba hilo   linataka   kunyanganywa na bwana sudi kwa lengo   la yeye kutaka kuwakodisha wanakijiji hao.   Mwanakijiji mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Hashimu Idd Ri

CHUO CHA MAZINGIRA CHAKABILIWA NA UCHAKAVU W MAJENGO.

CHUO cha  Sayansi ya   Afya  ya Mazingira  kilichopo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma kinakadiliwa na uchakavu mkubwa wa  miundo mbinu ya chuo hicho na kutishia afya  wanachuo chuoni hapo.  Akitoa taarifa mbele ya mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir Shekimweri mkuu wa chuo hicho  bwana  Rogasian Tarimo  alisema  chuo hicho ambacho ni tawi la chuo kikuu cha  Muhimbili(MUHAS) kinachotoa elimu ya AStashahada ya Aya ya mazingira. Bwana Tarimo alisema  chuo hicho chenye wanachuo  54 kinakabiliwa na uchakavu mkubwa wa miundo mbinu  na kutishia afya za wanachuo chuoni hapo . Aidha Tarimo alisema  chuo hicho tangu kifanyiwe ukarabati mdogo mwaka 2002  hakijafanyiwa  ukarabati tena na kupelekea miundo mbinu mingi kuchakaa  na kushidwa kufanya kazi kiufanisi  kutokana na kuchaa sana . Alisema “sisi ni maafisa wa afya ya mazingira  ninaowafundisha ni wataalamu wa afya ya mazingira sasa uchakavu huu hauendani na maudhui ya chuo kwa maana miundo mbinu ya vyoo imechaa,vyumba vya ma

SERIKALI YAWAPA MTIHANI WAKUU WA SHULE MPWAPWA

SERIKALI wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma  imewataka wakuu wote shule zote za kidato cha sita zilizopatiwa fedha za ukarabati  kuthaminisha ukabarabati wa shule hizo  sambamba na uboereshaji wa elimu katika shule zao. Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa  Jabir Shekimweri alipotembelea  shule hizo kwa ajili ya kuangalia hali halisi ya ukarabati unaoendelea  katika shule hizo. Shule zilipatiwa fedha za ukarabati  katika shule  za kidato cha sita ni Mpwapwa Sekondari ,Mazae Sekondari,Berege sekondari na  Kibakwe Sekondari. Shekimweri alisema  hakuna zaidi kwa shule hizi kutoa shukrani kwa serikali zaidi ya kupandisha kiwango cha ufaulu  katika shule zote ambazo zimepatiwa fedha za ukarabati. “haiwezekani shule zinapendeza zinanga’aa lakini ufaulu unakuwa chini hivyo  wakuu wa shule  na walimu mjipange  sasa uzuri wa miundo mbinu hii ya shule iendane  na viwango vya elimu vinavyo tolewa shuleni hapa tunataka kusiwe na  division four wala three hapa tuanzie div

VIJANA WACHANGAMKIA NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA.

Idadi kubwa ya vijana wajitokeza kuchukua fomu   za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi   wa ndani ya   Chama cha mapindinduzi (CCM)   Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma. Katibu wa chama hichoi wilayani   Mpwapwa mkoani Dodoma Bi.Rukia   Hassan amedhitisha hilo kuwa idadi kubwa wa watu waliochukua fomu za kugombea   nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama ni kubwa ni     vijana .   Bi Rukia amesema kuwa mchakato wa uchaguzi ulioanza   mwezi April mwaka huu katika ngazi za mashina   na kudhibitisha kuwa fofauti na miaka   iliyopita ambapo wanachma wengi wamejitokeza kugombea nafasi zauongozi ndani ya chama kwa kile alicho kisema kuwa ni kiashiria   cha Imani ya wanachama kurudi kwa chama. Aidha amesema pamoja na kukua kwa imani ndani ya chama pia ni kuongezeka kwa uelewa Demokrasia   ndani ya chama pia kupunguza vikwazo vilivyo kuwa   vinakuwa   kipingamizi   kikubwa cha wanachamakuingia katika nyadhifa mbalimbali   ikiwemo Rushwa,Kujuana   na Upendeleo. Pia Bi Rukia