MAHAKAMA ZADAI KUINGILIWA NA SERIKALI KIUTENDAJI

Omana Gouth na Noel  Stephen  Mpwapwa

Imeelezwakuwa  katika utendaji  wa kazi wa Mahakama za Jamahuri wa Muungano wa Tanzania haziko huru kama inavyo ainishwa katika Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

 Hayo yamebainishwa  na wajumbe wa mdahalo wa katiba uliofanyika  katika Ukumbi wa ccm Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma ulioendeshwa na Mtandao wa Asasi za  Kiraia NGOMNET Mpwapwa.

Akichanngia mada katika mdahalo huo  mmoja wa washiriki Bwana JEMSI KAREIMAHA  hakimu mfawidhi wa mahakama  wa wilaya ya Mpwapwa  alisema katika utendaji wa  kazi katika mihimili  mitatu ya dola  ambayo ni Serikali,Bunge na Mahakama kunaonekana kuwa serikali inakuwa na madaraka makubwa kuzidi mihimili mingine katika utendaji  kazi wake kutokana na muhimili mmoja kuutegemea muhimili wa mahakama kwa kuwezeshwa  kifedha na vitendea kazi.

Aidha Bwana Kareimaha alidai kuwa katika utendaji wa kazi wa kutoa maamuzi ya kimahakama Rais anaweza kutengua  hukumu iliyo iliyotolewa na hakimu au jaji kwa madaraka aliyokuwa nayo  kikatiba kitu alichosema kinaleta utata wa kiutendaji.

Pia  akiongezea  mchangiaji mwingine bwana Kandido Mnemele mwakilishi wa kundi la walemavu wilayani mpwapwa (shivyawapwa) alisema kuwa katiba hiyo bado haifahamiki kwa wananchi wa vijijini na wala hawaijui rangi yake, na imeandikwa bila kuzingatia uhitaji wa makundi maluum kama walemavu wa macho,kwa kuandika  katiba ya maandishi ya nukta nundu.

Bi ELLY MAKALA  afisa wa Tasisi wa kuzuia na kupamabana na rushwa nchini PCCB alisema kuwa watanzania bila kubadilisha  mtazamo  wa kuwa na maadili na kufuata kanuni na sheria za kazi katiba mpya haiwezi kuwa jawabu la matatizo ya watanzania  bila ya viongozi kuwa waadilifu.

“Hata tusemeje na tutunge sheria nyingi kiasi gani hatuwezi kutataua matatizo ya watanzania  bila kubadilisha mtazamo  wa viongozi kuwa waadilifu, jawabu la matatizo ya watanzani yamo mikononi mwao wenyewe kwa kujenga moyo wa kushiriki,kupanga na kufuatilia  mipango ya kimaendeleo na kuwawajibisha viongozi wabadhilifu’’  Alisema bi makala.

Akitoa mada katika mdahalo huo mmoja wa wawezeshaji Daktari Sinda HUSSEN SINDA  kutoka chuo kikuu cha Dodoma alisema kuwa  TANZANIA  haina Dira na dhima juu ya mstakabali wa Taifa  juu ya siasa ujamaa na kujitegemea kuwa wanachi hawajui wanafuata siasa ya mlengo wa namna gani,kibepari,kibwenyenye,ua siasa ya ujamaa na kujitegemea.



Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.