Posts

Showing posts from July, 2020

DC MPWAPWA AHIMIZA TEKNOLIJIA ITUMIKE KUPUNGUZA MALARIA NCHINI.

Image
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Mpwapwa.   Mkuu  wa wilaya ya Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, Mh. Jabir Shekimweri, amewaagiza wataalamu wa mifumo ya teknolojia hapa nchini kuang alia uwezekano wa kuitumia mifumo hiyo kwa kutoa elimu ya namna ya kudhibiti malaria hasa katika maeneo ya vijijini. Mh. Shekimweri ameyasema hayo wilayani Mpwapwa alikupowa akizindua mpango wa matumizi salama ya vyandarua vyenye dawa vilivyotolewa na Serikali kwa lengo la kutokomeza malaria hapa nchini mafunzo yaliyofanyika mjini Mpwapwa. Mkuu wa wilaya hiyo  amesema kwa nyakati  hizi, simu za mikononi zenye mitandao ya kijamii zimeenea kila mahala, hivyo ikiwepo namna nzuri ya kufikusha ujumbe utakaosaidia wananchi kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguuka, kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza mazalia ya mbu wanaosababisha maambukizi ya Malaria. Mafunzo hayo yamewashirikisha wataalamu mbalimbaalia kutoka wilaya za Kongwa na Mpwapwa mkoani Dodoma wakiw