Posts

Showing posts from August, 2017

DC atangaza vita na waharibifu wa mazingira mpwapwa.

  Mkuu wa wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma Jabir Shekimweri ametangaza vita na watumishi wa serikali watakao bainika katika   kuihijumu serikali   katika vita ya kupambana   na uharibifu wa mazingira Mpwapwa. Shekimweri aliyasema hayo ofisi kwake alipo kuwa akiongea na   waandishi    juu   mikakati ya kuikomboa wilaya hiyo juu ya uharibifu   wamazingira. Mkuu wa wilaya hiyo alisema     kupitia kamati ya ulinzi na usalama imebaini baadhi ya watumishi wa serikali wamekwa wakihusika katika uharibifu wa mazingira kwa   kuwa na vibali feki ya kuchana mbao . Aidha alisema   watumishi wote waliotuhumiwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kinidhamu na hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakama   kujibu tuhuma zinazo wakabili. “Inasikitisha kuona watumishi wenzangu wa serikali   kujikita   katika sula la uharibifu wa mazingira ,kwa hili sitakuwa na uvumilivu hata kidogo katika mazingira mimi nina zero tolelance lazima wote wachukuliwe hatua na wafikishe mahakamani.”aliongea  

WANAFUNZI WA AWALI IDILO MPWAPWA WASOMEA CHINI YA MITI.

Image
WANAFUNZI WA awali katika shule   ya msingi   Idilo   wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma   huwalazimu kusomea chini   ya miti kutokana na   uhaba wa vumba vya madarasa sheleni hapo. Wanafunzi hao waliokutwa   na majira   wakiwa wamekaa   kwenye viti   vya matofali huku wakiwa chini miti na darasa linaendelea. Ofisa elimu kata ya Mazae Bwana Betweli Sanga     alikili wanafunzi hao kusomea chini ya miti kitu alicho sema kinasababishwa   na uhaba wa   wa vyumba vya madarasa   katika shule hiyo. Sanga   alisema kwa   sasa shule hiyo inavyumba vya madarasa   7 wakati mahitaji ni   vyumba 10 na kupelekea kuwa   upungufu wa vyumba   vitatu   vya madarasa   shuleni hapo. Sanga alisema kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 290 wakiwamo wavulana 129 na wasichana 120lakini inavyumba saba vya madarasa. Aidha Sanga alisema pamoja na uhaba wa vumba vya walimu pia shule hiyo inakabiliwa na chanagamoto ya nyumba za walimu,matundu ya vyoo,pamoja na vifaa vya kufundishia Kufuatia hali hiyo u

DC agundua chang za maji mpwapwa.

Image
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akikagua baadhi ya mitambo ya maji katika kisima cha Kiombo. ZAIDI ya wakazi   29,422 wa mji wa mpwapwa na viunga vyake hutumia maji machafu   yasiyo tishia kutokea kwa magonjwa ya mlipuko   yanayosababishwa na matumizi maji maji machafu. Hali hiyo imebainishwa na Mkuu wa wilaya ya   Mpwapwa mkoani Dodoma bwana Jabir Shekimweri   baada ya kutembelea vyanzo vya maji vinavyo saidia   kusambaza   maji katika mji wa   Mpwapwa. Pia Shekimweri abaini   changamoto lukuki zinazosababisha Mji wa Mpwapwa kuto kuwa na maji ya uhakika japo ya kuwa na mradi   mkubwa wa maji ulioghalimu jumla ya shilingi billion4. Aidha changamoto zilibainishwa na mkuu wa wilaya hiyo ni maji yanayotumiwa na wakazi mpwapwa ni machafua ambapo tumbili,Ngedele na wanyama wa poli kuyatumia na kuoga   humo kutoka na chanzo hicho kutokuwa   na uzio   wa kuweza kuzuia wanyama kuchafua kwenye vyanzo hivyo. Pia ufanisi hafifu wa mradi   wa maji chumvi ujulikanao

HAKI ELIMU WATAMBULISHA MKAKATI WA MIAKA MITANO MPWAPWA.

SHIRIKA   lisilo kuwa   la kiserikali linalojihusisha   na ushawishi katika kuboresha Mazingira ya Elimu hapa nchini   la Haki Elimu limeiomba serikali kuendelea kushughulikia chamngamoto zinazo ikabili Elimu kwa sasa ili kuweza kuwa   wataalamu wenye tija siku za mbeleni. Kauli hiyo ilitolewa na wadau wa elimuwilayani hapa   katika kikao cha pamoja na   shirika la Haki Elimu   walipokuwa wakitambulisha mkakati wao wa miaka mitano utakao fanywa na shirika hilo juu ya   kuweza kuinua   Elimu hapa nchini. Ofisa Programu   wa shirika hilo bwana Frolige   Lyelu   amesema pamoja na serikali kuonyesha   nia dhabiti ya kuikomboa elimu   hapa nchini lakini kuna bado baadhi ya changamoto ambazo zinatakiwa kumalizwa na ngazi za chini   kuliko kuendelea kuisubiri serikali . Frolige alisema   Mpango wa Elimu bila malipo umeweza kuongeza hamasa ya watoto wengi kuandikishwa   darasa la kwanza na wanao jiunga kidato cha kwanza idadi imekuwa ikiongezeka kila mwaka kitu alichosema kuwa   ki