KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

 Mpwapwa. Habari.


Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi Sophia Kizigo  akiongea kwenye mkutano kazi wa RUWASA na wadau wa maji uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Afya.(picha na Emanuel Uronu(Vaino)

Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma Bi Sophia Kizigo  amezitaka jumuiya za watumia maji  kuweza kuunganisha nguvu  za jumuiya moja na nyingine ili kuweza kutoa huduma   bora  kwa wananchi.

Kizigo ametoa Rai  hiyo wakati wa kikao kazi cha wadau wa maji kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha Afya mjini hapa   kilicho wajumuisha  Viongozi wa jumuiya za watumia maji  watendaji wa kata na vijiji napamoja na  madiwani wa kata husika ,

Kizigo amesema pamoja na serikali ya awamu ya sita kuweka dhamira thabiti ya kumtua  mama ndoo kichwani  lakini bado  jamii husika imeendelea   na uharibifu wa mazingira unaotishia uendelevu wa miradi mikubwa ya maji  inayowekezwa na serikali.

Kupitia changamoto hiyo  ametoa siku 14 kwa madiwani wote wanasiasa na baadhi ya watendaji wa kata na vijiji wanaowakingia  vifua waharibifu wa mazingira  kuchukuliwa hatua za kisheria  kwa wote.

Aidha amedai jumuiya za watumia maji  kuweza kufuata miongozo,kanuni na taratibu za utunzaji wa fedha zitokanazo na miradi ya maji katika vijiji, na kata ili kuweza kupunguza migogoro  ya matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maji ‘’nina taarifa nyingi juu uendeshaji mbovu wa jumuiya hizi sasa kwa vile mmejengeana uwezo  naamini mtaenda kubadilika  wale ambao hawatabadilika  tutajua za kufanya” aliongea 


 Baadhi ya wadau wa maji wakifuatilia mjadala wa huduma za maji  ulioendeshwa na RUWASA Mpwapwa.

eneja wa Ruwasa  Wilaya ya Mpwapwa   mhandisi Cyprian Warioba  alisema  kwamba  lengo la kikao hicho  ni  kuwajengea uwezo  viongozi wa  jumuiya za watumia  maji ili kuweza kusimamia miradi ya maji na kuifanya kuwa yenye uendelevu  na yenye tija kwa jamii inayolenga kupunguza changamoto  ya upatikanaji wa maji kwa jamii.

Hata hivyo Mhandisi Warioba   alisema mpango wa kuunganisha  jumuiya za watumia maji  utaweza kuongeza ufanisi na kupanuka kwa huduma Zaidi lakini itapunguza gharama za uendeshaji  na kuifanya miradi mingi kuwa na tija .

Amedai kwamba kwa sasa wilaya yaMpwapwa imeingia kwa Mpango wa lipa kutokana na matokeo hivyo  lazima jumuiya hizo kuzingatia taratibu na sheria  za uendelevu wa miradi. 


Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Mpwapwa Cyprian Warioba akiongea kitu na wadau wa Maji katika kikao kazi kilichofanyikakatikaukumbi wa Chuo cha Afya.

Mhandisi Warioba alisema kwa mwaka wa fedha   2023/2024 Serikali kupitia  wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa)Mpwapwa  imepanga kutekeleza miradi ya maji 15 katika maeneo mbalimbali  itakayogarimu jumla ya shilingi   2,681,190,153.00  “na idadi ya watu wanaopata Huduma ya  Maji Safi na Salama mpaka  sasa ni watu wapatao 248,727 ambapo  Sawa na asilimia 65.05.makadirio ya watu wapatao 320,891”

Mwenyeiti wa jumuiyaya watumia maji kautoka kata ya Chipogoro   bwana Msafiri  Mgonela (Punda wa Yesu)  alisema katika kijiji chao wakati anaingia madarakani  alikuta kijiji kizima kina vituo vine vya kuchotea maji na watu waliokuwa  wameunganishiwa maji majumbani  walikuwa watano “mpaka sasa watu waliunganishiwa maji majumbani ni themanini na watano  kutoka kwenye watano,na kuongeza vioski vya kuchotea maji kutoka vitano hadi kumi na viwili lakini tasisi zote tumeshaziunganishia  maji.

mwisho.


Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA