Posts

Showing posts from October, 2017

JAMII YAFICHA TAARIFA ZA UKATILI.

MTANDAO wa polisi wanawake wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma umesema kasi ya ukatili kwa watoto inasababishwa na jamii kuficha taarifa za vitendo hivyo. Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa dawati lá njisia katika kituo cha polisi wilayani hapa Bi Elfrida Mapunda katika maadhimisho ya miaka kumi ya kuanzishwa kwa dawati hilo. Bi Mapunda amesema kuwa vitendo vya ukatili vinavyodhidi kushika kasi vinasababishwa na jamii kuzidi kuvifumbia macho vitendo hivyo au kamalizana kienyeji bila kufuata sheria na bila kuangalia madhara. Aidha Bi Mapunda ameitaka jamii kwa kusaidiana na jeshi lá polisi kuweza kushirikiana katika kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto na wanawake. Pia amesema katika kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao huo kumeongezeka kwa taarifa za ukatili ambazo hapo awali zilikuwa zinafichwa kutolewa. Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho bi Selina Chimwaga amesema kuwa kuwa kundi kubwa lá watoto hao wenye mtindio wa ubongo wanakabiliwa na chan

DC MPWAPWA AWAHADHARISHA WAKULIMA PWAGA.

Mkuu wa wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma  bwana Jabiri Shakimweri  amewataka wananchi  wa vijiji vya Pwaga na Mingui  kuto kuuza ardhi kiholela hasa katika kipindi hiki cha ujio wa serikali mkoani Dodoma Shakimweri aliyasema hayo juzi alipokuwa akifungua mafunzo ya  kwa wakulima wa vijiji vya pwaga  na Mingui wilayani Mpwapwa yaliyofadhiliwa na Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge  (MKURABITA) juu ya kuweza kuitumia ardhi kama  rasilimali muhimu kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na  Taifa kwa ujumla. Aidha Shakimweri amesema kuwa mala baada ya serikali kuanza kuhamia Dodoma kumeibuka baadhi ya watu  wanao zunguka katika wilaya zote za mkoa Dodoma  kununua maeneo ya watu kwa bei nafuu  na kuwaacha  wakazi wa maeneo hayo  katika hali ya umaskini  na kutishia kuwapo katika  mogohoro ya ardhi. Mkuu wa wilaya hiyo amesema lazima wanannchi hao  kuweza kutumia fursa za  hati za kimila za ardhi  kwa kuweza kuongeza dhamani ya ardhi  kwa kupanda mazao ya biashara y