Posts

Showing posts from 2019
Image
Mwl.Augusta Lupokela kaimu mkurugenzi msaidizi wa mafunzo ya ualimu ,Wizara ya Elimu Sayansi na Tecknolojia. MBUNGE wa Jimbo la Mpwapwa   Mhe George Lubeleje (Seniour MP) ameiomba serikali kuweza   kutenga Bajeti ya kutosha    katika sekta ya michezo   nchini ili   kuwezesha kuwezesha tanzania kufanya vizuri katika nyanja ya michezo   katika soko la ndani na nje ya michezo na ulimwenguni. Mhe Lubeleje aliyasema hayo   juzi alipokuwa akifungua Kongamano la Michezo   la vyuo vya ualimu kanda ya kanda linalofanyika katiia chuao cha ualimu   kilichopo Mpwapwa Mkoani Dodoma. Mhe Lubeleje alisema kwa sasa   nchi ya Tanzania inashidwa kufanya vizuri katika nyanja za michezo kutokana na   serikali kushidwa kuwekeza vya kutosha katika sekta hii ya michezo   ambayo inaoneka kukua kwa kasi   hapa nchini. Aidha amesema kwa sasa soko la michezo hapa nchini limeonekana kushika kasi kubwa na   kuwajumuisha vijana wengi na hivyo kwa kuona umuhimu huo serikali ya awamu ya tano imeamu

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIKA 30 JELA KWA KOSA LA KULIMA BANGI.

Image
Bwana Odeni Mwikola   akiwa chini ya ulinzi wa Polisi akisindikizwa kwenda kuanza  Maisha Mapya Jela . Mahakama ya Hakimu mkazi ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imewahukumu kifungo cha miaka thelani jela bwana Oden Mwikola (32) baada ya kupatikana na hatia ya kulima zao haramu la Bangi . Kesi Hizo zilizo kuwa zinasikilizwa na hakimu mkazi bwana Pascal Mayumba wa mahakama Hiyo ya wilaya.  Hakimu mayumba aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa Oden Mwikola alitenda kosa hilo kinyume na sheria namba 11 kifungu kidogo cha 1(a)na(b)ya kuzuia madawa ya kulevya   sura 5 ya mwaka  2015 ambapo walilima shamba la Bangi lenye ukubwa wa  heka moja.  Hata hivyo Mayumba  aliiambia Mahakama kuwa kesi hiyo iliyopewa nguvu na mashahidi 5 na vielelezo vitatu ikiwemo hati ya ukamataji, maelezo ya onto na taarifa ya mkemia mkuu iliyo thibitisha kuwa mmea ulio patikana Katika shamba la Bwana Odeni ilikuwa ni Bangi.  Pia alisema kutokana na vielelezo na ushahidi ulio

MPINA WAKULIMA BARUA WAKURUGENZI NCHINI,Walioshidwa kukarabati Majosho.

Image
MPWAPWA KITAIFA /KILIMO NA MIFUGO. Waziri wa mifugo na uvuvi bwana Luhaga Mpina amesema anatarajia kuwaandikia barua za kusudio kuacha kukusanya mapato yote yatokanayo na mifugo kwa Halmashauri zilizo shidwa kutekeleza Agizo lake la azimio la Chato la kukarabati Majosho mabovu ili kuongeza huduma za uogeshaji kwa wafugaji. Waziri Mpina ametoa Agizo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma alipo kuwa kwenye ziara ya kikazi ya kutadhimini zoezi la uogeshaji limefikia Wapi  Tangu lizinduliwe mwezi November mwaka 2018.  Waziri Mpina amesema Katika uzinduzi huo huko Chato alitoa Maagizo manne kwa Halmashauri zote nchini kuyatekeleza kitu alicho kisema kuwa baadhi ya Halmashauri zimetekeleza na zingine hazijatekeleza.  "Nilipokuwa Chato nilitoa maagizo kuwa kila Halmashauri itenge asilimia 15 ya mapato yake ya ndani kwa zitakazo rudi kwa wananchi kuboresha huduma za mifugo nchini. Pia nilisema Majosho yote mabovu yakarabatiwe ili kuongeza fursa za wananchi kuogesha mifugo ya