Posts

Showing posts from March, 2020

DC MPWAPWA AMESEMA HAKUNA MTU ATAKAYE KUFA KWA COVID 19KAMA WATAZINGATIA MAELEKEZO YA WATAALAM.

Image
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri  Akiongea na Mwandishi wa habari hizi ofisi kwake. Picha na Mpwapwa Habari. Na Stephen Noel . Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Bwana Jabiri Shekimweri amesema wananchi wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa CORONA CIVID- 19   na wasitishwe na mamneno ya mitandao juu ya ugonjwa huo. Mkuu wa wilaya ameyasema hayo jana ofisi kwake akifanya mahojiani na   na mwandishi wetu juu ya mkakati wa wilaya thidi ya kujikinga na    maambukizi ya ugonjwa   huo ambao   kwa sasa umekuwa ni janga la kimataifa. Shekimweri amesema   lazima   wananchi   waelewe na kuendelea kuchukua tahadhari thidi ya ugonjwa huo   ambapo kama “ kama wilaya tayari tumesha fanya uhamasishaji katika makundi yote yanayo tuzunguka   wakiwemo wafanya biasahara bodaboda   masokoni makanisani na misikiti juu ya kujenga uelewa kwa jamii na njia za kujinga    na kuwakinga wengine.   Mganga mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Erich