DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.


 Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi Sophia Kizigo akifungua kikao   cha wadau wa Ulinzi dhidi ya Mtoto na ukatili wa kijinsia kilicho wezeshwa na Jukwaa la utu wa Mtoto CDF wilayani Mpwapwa.



 Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika la utu wa Mtoto CDF Koshuma Mtengeti akichangia jambo  katika kikao cha kujadili ulinzi wa Mtoto wilayani Mpwapwa.

 Stephen Noel-Mpwapwa. 
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bi Sophia Mfaume Kizigo ametoa  amri kwa maafisa Elimu wote ndani ya wilaya hiyo kuhakikisha shule zote za Msingi na sekondari zinakuwa na walimu walezi kwa lengo la kupunguza vitendo vya ukatili kwa watoto wawapo shuleni.
Mkuu wa wilaya hiyo ametoa agizo hilo kwenye mkutano wa Siku moja uliondaliwa na Asasi ya kiraia jukwaa la utu wa mtoto  CDF  iliyo kutanisha Wadau wote wanao fanya  afua za kumlinda mtoto na kujali ustawi wa mtoto.
Amesema Ili kuhakikisha watoto wanakuwa Kwenye mazingira ya usalama lazima kunakuwapo na  watu wanao ratibu  kero zinazo wakabili watoto au pindi wafanyiwapo ukatili  nyumban au eneo la Shule.
Bi Mary Jackoson Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake wilaya ya Mpwapwa  akichangia jambo katika kikao cha Jukwaa la utu mtoto kilichofanyika  katika umbi wa ofisi ya Mkuu wa wilaya  May 17.2023.

 

"Sasa naagiza kwa maafisa Elimu wote Msingi na sekondari kuwa ifikapo kesho shule zote ziwe na matron na Patron  hili halihitaji  mpango kazi lifanyiwe kazi mala moja"Alieleza Kizigo.
Kaimu Ofisa Elimu sekondari  bwana  Ally Akida   amesema Kwa Sasa Mpwapwa ina Shule 33 za sekondari ambazo   jumla ya wanafunzi 17,249  na wanafunzi waliopanga vyumba (mageto) ni wanafunzi 1204 ambao hujilea wenyewe na wapo Katika hatari kubwa ya kufanyiwa ukatili kutokana na mazingira wanayo ishi.
Afisa Elimu Msingi   Bwana Jackson Mpankuli   amesema  kuhakikisha watoto wanakuwa Katika usalama  wa ni wajibu wa  wazazi,/ walezi na walimu wanashirikiana  Katika malezi  ya watoto wao.
Ofisa  wa dawati   WP  2420 Sanjeti Magreth   amesema kuanzia mwezi March  jumla  makosa 15  ya ubakaji yalilipotiwa katika kituo cha polisi ,  makosa matano ya ulawiti yalilipotiwa na makosa mawili ya kuwapa wanafunzi mimba yalilipotiwa  kuanzia mwezi March 2023.

 

Kwa upande Wake mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la utu wa mtoto    Koshuma Mtengeti alisema tangu shirika hili lianze kufanya kazi katika wilaya hiyo mwaka 2017 wamefanikiwa kupunguza vitendo vya ukatili wa Kijinsia  kwa Jamii  ikiwemo kwa watoto wa kike,pia amesema wameongeza uelewa kwa jamii ambapo umesababisha  taarifa za vitendo vya ukatili kulipotiwa Katika vyombo vya kutoa maamuzi. 
Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.