SHARIF AHMED RAIS WA SOMALIA AFANIKISHA MPANGO WA AMANI

Mei 22, 2012
Rais wa Somalia na waziri mkuu walihutubia mkutano wa Mpango huko Addis Ababa mnamo Jumatatu (tarehe 21 Mei), wakisisitiza umuhimu wa kusaidia mpango wa mpito na maendeleo yake. Mtandao wa habari wa Garowe Online ya Somalia iliripoti.
Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed alibainisha mafanikio ya usalama katika kupambana na al-Shabaab. Waziri Mkuu Abdiwel Mohamed Ali alisema kuwa licha ya vizuizi katika kuchagua wajumbe wa baraza hili, mchakato utaendelea ili Serikali ya Mpito ya Shirikisho ifikie mwisho mwezi Agosti.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia Augustine Mahiga alikuwa mwenyekiti wa mkutano huu na kutoa wito kwa wanasiasa, dola na watia saini kufuata mkataba uliosainiwa huko Garowe, Galkayo na Mogadishu. Pia alitoa wito kwa viongozi wa Somalia kudumisha uadilifu katika mchakato wa uchaguzi wa Bunge la Katiba, ambalo litahakiki katiba mpya iliyopendekezwa.

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.