ASKOFU AZUNGUMZIA UTEUZI WA MAWAZIRI,USHUKE MPAKA CHINI

Askofu Nyaisonga akiwaonyesha waumini Biblia Takatifu ndani ya ibada .picha na Stephen noel

Na Stephen noel mpwapwa


Askofu wa kanisa katoliki jimbo la Dodoma Mhashamu Baba ASKOFU GELVAS NYAISONGA amesema kitendo kilicho tokea kwa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ni kukua kwa misingi ya demokrasia na uwajibikaji kwa jami na viongozi..

Hayo ameyasema wilayani mpwapwa siku mbili mara baada ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Jakaya kikwete kufanya mabadiliko katika Baraza la mawaziri Mhashamu ASKOFU Gelvas Nyaisonga ajitokeza hadharani na kuipongeza hatua hiyo kwa Rais na wananchi wa Tanzania pamoja na mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali Bwana Lodovicck Utto

Askofu NYAISONGA alisema kuwa kitendo hicho ni cha kishujaa na ni dalili ya kukua kwa demokrasia, uwajibikaji na kutadhiminiwa kwa viongozi na thamana za vyeo vyao kwa jamii kuwa s ni za muda tu na zinaweza kuchukuliwa wakati wowote .

Alisema kuwa viongozi wasijisahau kutumia ,,vibaya nakutambua kuwa vyeo walivyo pewa ni dhamana tu na watambue kuwa wanatadhimiwa na kufuatiliwa kwa hiyo ni lizima wawe waadiilifu katika kazi zao za kila siku,,alisema askofu naisonga.

Pia alisema kuwa kitendo kilicho tendeka kwa mawaziri ni lazima kishuke mpaka ngazi ya chini kwenye Serikali za mitaa kwa kutadhimini miradi inatekekelezwa na Halmashauri nyingi nchini kuwa chini ya kiwango na ndio inakuwa na madhara makubwa kwa jamii na watu wake hasa wale wa makundi ya pembezoni.

Akizungumza kuhusu kushuka kwa maadili katika jamii amesema ;
kuwa tatizo ni wazazi na walezi wamekuwa wamejikita zaidi katika mambo ya uchumi na uzalishaji na kijisahau katika malezi kitu kinacho pelelekea jamii inakosa malezi hasa watoto.

Kuhusiana na Muungano wa Tazania na Zanzibar Askofu yaisonga alisema Watanzania hawana budi kuulinda muungano kwa nguvu zao zote kwani ni historia pekee ambayo Tanzania ambayo wasisi wa taifa hili waliiacha kuonyesha muafaka wa kitaifa.

Alikemea k wa baadhi ya wa TANZANIA ambao wanasema kuwa ni wanaharakati ambao wanataka muungano uvunjike alisema kuwa ukosefu wa ukomavu wa elimu ya muungano wa kitaifa.

Na aliwataka serikali kuweza kuruhusu muungano ujadiliwe katika mchakato wa katiba mpya ili uweze kupata maoni ya wananchi wanauzungumuziaje muungano na kama bado wanauhitaji na una manufaa kwao.

Alipokuwa wilayani mpwapwa Askofu Nyaisonga aliendesha misa Takatifu ya katoliki parokia ya mpwapwa na alitoa kipaimara kwa watoto wapatao 150, mjini hapo.


















Katibu wa CHADEMA MPWAPWA Bwana Fabiani Moke akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.

Na Stephen Noel Mpwapwa.
Katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) wilayani mpwapwa bwana FABIANI KOSMAS MOKE amesema wanajiandaa kuinyakua kata ya mpwapwa mjini mara baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo marehemu Noah Maiseli ccm kufariki dunia march 27,mwaka huu.

Bwana MOKE aliyasema hayo wilayani mpwapwa ofisini kwake alipo kuwa akizungumza na waandishi hwa habari kuelezea mikakati yao walio iweka juu ya uchaguzi mdogo unao talajiwa hivi karibuni wilayani hapo kwa lengo la kufidia nafasi iliyo achwa na diwani wa ccm kufariki dunia.

Katibu huyo alisema kuwa japo kuwa wilaya ya mpwapwa ni kongwe kwa umri lakini imekuwa nyuma kimaendeleo kutokana na mfumo uliopo katika Halmashuri hiyo kuwa na Madiwanai wa Chama kimoja kitu alicho kisema kuwa Madiwani wa ccm wanashidwa kuwajibishana wao kwa wao kwa dhana ya kulindana na kuoneana aibu.

Alitoa wito kwa wananchama wa mpwapwa kuwa waige mfano kwa wenzao wa mikoa ya Arusha,mara na mbeya kukipa ridhaa chama cha chadema ili kiweze kukomesha ufisadi ulioweka kambi katika Halmashauri ya wilaya ya mpwapwa ili wilaya hiyo iweze kuwa ya kuigwa na yenye maendeleo mkubwa.
Aidha ofisini hapo kuliongonzana na baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi ccm kurudisha kadi za chama hicho na kuchukua kadi za chama cha demokrasia na maendeleo chadema ambpo katibu huyo alisema kwa muda wa miezi mitatu wameweza kuongeza wanachama wa ccm wapata 625. wengi wao wakiwa vijana na akina mama.

Pia bwana Moke Alisema siku za nyuma watu wa mpwapwa walikuwa wana mawazo duni juu ya vyama vya Siasa kuwa ni vyama ya kuleta fujo kitu alicho kisema kuwa sasa wananchi wamemamuka na wanataka maendeleo.

Akiongea mmoja wa akina mama ambae ni kada wa chama cha mapindizi siku nyigi na ambae hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa amechoshwa na chama hicho kuwa kwa sasa kimepoteza mwelekeo hivyo yeye kama mtu mzima ameanglia alama za nyakati na kuona kuwa ccm haina muda mrefu kuendelea kuendesh dora.
Akiongea mmoja wa vijana ambao walibadilisha fomu ya umoja wa vijana ccm nakuchukua fomu ya chadema bwana Mwinyi Liunda alisema kuwa chadema ndio chama cha Vijana ambacho kina mwelekeo wa kuonyesha mwanaga wa Tanzania hasa watanzania wanyonge na wa pembezoni zaidi.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo ya siasa wilayani mpwapwa bwana Edward Mwamakula alisema kitendo hicho cha wanachama wa ccm kuhamia chadema kipindi hiki kinaweza kikawa ni mchezo mchafu kwa chadema ili kuwarubuni ifikapo uchaguzi wawe na kundi kubwa la watu lisilo kuwa na manufaa kwao na kura wakapigia ccm hivyo chadema wanapaswa kuwa makini alisema bwana Edward.

Mchakato wa kuanza kuigombania kata hiyo itanza hivi karibuni mara baada hatua zote za kisheria kukamilika kwa siku 90 za kata hiyo kuwa wazi tangia tarehe 07.march mwaka huu diwani kufariki huko nchini India kwa ugojwa wasaratani ya damu.

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.