Posts

Showing posts from March, 2018

BABA AMBAKA MWANAE WA MIAKA 12 NA KUMMPA MIMBA.

Mtu mmoja   aliyefahamika kwa jina la Jemsi Leuna mkazi wa kijiji cha Chitemo wilaya   ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma    amefikishwa mbele ya hakimu makazi mfawidhi   bi Nurupedesia Nassar kufutia tuhuma ya kumbaka na kummpa mimba mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 12 mwanafunzi wa darasa nne. Mwendesha mashitaka wa polisi Bwana Michael Joseph   aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo akitambua kuwa   huyo ni mtoto wake wa kumzaa aliweza kumbaka   na   kutenda kosa hilo kinyume na   kifungu cha namba 130 kifungu kidogo(1) na kifungu 131kifungu kidogo(1)iliyo fanyiwa malejeo mwaka 2002. Bwana Machael   aliiambia mahakama   kuwa kosa la pili   ni kummpa mimba mwanafunzi darasa la nne kinyume na   sheria ya Elimu namba 353 kifunfu cha 60Akifungu kidogo cha kwanza   iliyofanyiwa malejeo mwaka 2016. Mtuhumiwa alipo ulizwa juu ya tuhuma hizo alikanusha kutenda kosa    na kesi yake iliahirishwa   hadi itakapo somwa tena march 26 mwaka huu.

WALEGWA WA TASAF MPWAPWA WATAKIWA KUBADILIKA.

Image
Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa Tasaf wilayani Mpwapwa bi Jaribu  Mtwange  akiwa kwe nyumba yake kabla hajajenga  nyumba. Ofisa ufuatiliaji wa TASAF wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma bwana Hosea Sichone   amewataka wawanufaika wa mpango wa kunufaika na kaya maskini   Tassaf wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma kutimiza masharti ya Mpango huo ikiwemo kusomesha watoto na kuboresha huduma za afya ili kuweza kuwa na mafanikio yaliyo kusudiwa ya mpango huo. Sichone aliyasema    hayo mjini hapa katika zoezi la uhuwilishaji wa fedha katika malipo ya fedha kwa walegwa kwa kipindi cha   mwezi March –Apri 2018.   Aidha Sichone amesema   kumekuwa na upotoshaji mkubwa   kutoka kwa jamii kuwa serikali inatoa fedha hizo bure tu kwa walegwa kitu alicho kisema kuwa   madhumuni ya   mpango   huo ni kuziwezesha kaya maskini   sana kuongeza matumizi muhimu kwa njia endelevu   kuziwezesha kaya hizo kuwa na pesa za matumizi wakati   wa hari, Ameongeza kuwa   pia madhumuni mengine   ni kuwekeza katika r

MAENDELEO YA MPWAPWA YAMNYIMA USINGIZI DC,AWATAKA WACHIMBAJI WALIPE KODI.

Image
SERIKALI wilayani Mpwapwa Mkoni Dodoma imewataka wachimbaji wadogo wa madini   Kuweza kulipa kodi ya   serikali ili kuweza kufikia Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kati   ifikakapo 2015. Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir Shekimweri   alipokuwa akifunga   mafunzo ya siku moja yaliyo andaliwa na shirika la wachimbaji madini Wanawake Tanzania(TAWOMA) Shekimweri alisema kuwa kuwa Mpwapwa pamoja na kujaliwa   madini ya aina nyingi na yadhamani lakini wilaya hiyo aiendani   na maendeleo yalikuwanayo   kitu alichosema kuwa kinatokana   na matumizi mabaya ya rasilimali hizo au usimazi mbovu wa rasilimali hizo   au matumizi mabaya mali hizo ambayo ni za watanzania wote. ALISEMA “ukiangalia Mpwapwa haiendanani na hostoria   ya wilaya hiyo kimaendeleo japo kuwa na kuwa na Neema ya wilaya   hiyokujaliwa   vitu vingi sasa nataka mlipe kodi ya serikali ilitufikie uchumi wa viwanda na uchumi wa kati ifikapo 2025,lakini tukilipa kodo kwa tutaboresha miradi

WANANCHI WAMKATA MAPANGA MTUMISHI WA HALMASHAURI,KISA KIPINDUPINDU.

Jeshi la polisi wilaya   Mpwapwa Mkoani Dodoma   linawashilikia watu wanne   wa kitongoji cha Isalaza kijiji cha Igoji II   kwa tuhuma za   kumjeruhi mtumishi wa Idara ya afya   halmashauri ya wilaya bwana   Yusuph Ridhiwani ofisa afya akiwa kazini . Tukio hilo    lilitokea march 03 mwaka huu katika kitongoji cha   Isalaza kijiji cha Igoji ii   wilaya ya Mpwapwa na mkoa Dodoma   baada ya   maofisa afya   wa halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa kwenda kwenye oparasheni ya kudhibiti kipindupindu. Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma bwana Giles Mroto amethibisha kutokea kwa kutukio hilo    na amesema chanzo cha   mtumishi huyo kujeruhiwa na siraha za jadi ilikuwa ni   waananchi kuto taka kusumbuliwa katika oparesheni ya kuzuia kipindupindi   ambapo kwa Mpwapwa ugonjwa huo umedumu kwa zaidi ya miezi mitano sasa tangu uingie mwezi nov mwaka jana. Akiwataja watu wanaoshikiliwa na jeshi alisema ni mwenyekiti   wa Igoji II bwana Gelezi Mlowela,Bahati Mwinyi holo,Eda Cholingo na Elei Ud

WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA DODOMA.

Image
Jeshi la polisi mkoani Dodoma limekamata wahamiaji haramu 64 ambao ni raia wa Ethiopia pamoja na madereva wawili waliokamatwa katika eneo la Chenene wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakitokea nchini Kenya kuelekea nchini Afrika kusini . Watu hao walikamatwa walikuwa kwenye roli lilosheheni mabox ya maji kwa ajili ya kuwaficha wahamiaji hao ambapo wamekutwa wakiwa na kiasi cha   fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 5. kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema wahamiaji haramu wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za udanganyifu ambapo amewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za wahamiaji haramu wanaoingia nchini. Peter Kundy ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji mkoa wa Dodoma amesema jeshi la uhamiaji mkoa wa Dodoma limejipanga katika kukabiliana na tatizo la uhamiaji haramu linaloonekana kushika mkoa wa Dodoma hapo. Kutokana na hayo wito unatolewa kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uwepo wa wahamiaji haramu nchini ili kudhibiti kitendo hicho.