Posts

Showing posts from June, 2020

WAGOMBEA WAKUMBUSHWA KUJIEPUSHA NA RUSHWA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI.

Image
. Mpwap wa .   Mkuu wa Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa wilayani Mpwapwa Bi Julieth Mtuy akiwakumbusha madiwani wa Halmashuri  ya Mpwapwa juu ya sheria ya Uchaguzi.  Mpwapwa Mkuu   wa tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani Mpwapwa   mkoani Dodoma   Bi Julieth Mtuy   amewatahadharisha   wanasiasa wanao taka kuwania   nafasi za ubunge na udiwani katika   Majimbo ya     Mpwapwa   na Kibakwe kutojihusisha   na vitendo vya rushwa wakati wa kuelekea katika chaguzi     mkuu. Mtuy ameyasema hayo na kuwakumbusha wagombea wa vyama vyote   kuto jihusisha na vitendo vyovyote vya utaoji wa rushwa kushawishi au kumchafua   mgombea mwenzie kama inavyo elekeza sheria ya gharama za uchaguzi namba 6 ya 2010 kuanzia k ifungu 15,21-23 kinachomtaka mgombea kuweka wazi ghalama za uchaguzi   atakazo zitumia ikiwamo misaada zawadi na vitu ingine kama magari na   usafiri mwingine. Mtuy alisema bila kufanya hivyo   mgombea   atakuwa amevunja sheria hiyo na atat

SIMBACHAWENE ATAKA URASIMU WA WATAALAMU USIDHOFISHE JUHUDI ZA SERIKALI

Image
Na   Mohamed Mhina wa Jeshi la POLISI- MPWAPWA Waziri wa Nchi Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mhe Simbachawene kikabithi kitabu cha Ilani ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa mwaka 2015-2020 Kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (w)Mpwapwa George Chigwiye.   Wataalam wa masuala ya fedha kwenye Halmashauri za Wilaya hapa nchini,   wmetakiwa kuacha urasimu wakati wa kufanya   maamuzi ya matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali katika kutekeleza miradi   ya maendeleo iliyokusudiwa. Agizo hilo limetolewa   na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. George Simbachawene, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ya jimbo la Kibakwe kwa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dododma. Akikabidhi kitabu hicho chenye kurasa 34 kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpwapwa Ndugu George Chigwiye, Mh. Simbachawene amesema kuwa baadhi ya watendaji kwenye halmash

KAMATI YA MICHEZO MPWAPWA YAAHIDI KULETA MAPINDUZI YA MICHEZO

Image
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Mussa Shekimweri akiongea na kamati ya michezo haipo Pichani. MKUU wa wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma bwana Jabir Shekimweri   ameitaka kamati ya michezo ndani ya wilaya kuwa   daraja kati ya vilabu    na vyama vya michezo vya kiwilaya na kitaifa ili kuifanya Mpwapwa kuweza kurudi tena katika ulimwengu   wa Michezo. Shekimweri aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua kamati ya michezo ya wilaya ofisini kwake.    Katika nasaha zake Mkuu wa wilaya kwa kamati hiyo alisema Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya zilizokuwa zikitamba katika   ulimwengu wa michezo na kuwa na timu kama   Waziri mkuu,Mjimpwapwa, na timu zingine za madaraja ya chini . Alisema siku za hivi karibuni   Mpwapwa imekuwa   haifanyi vizuri katika sekta ya michezo kutokana na sababu nyingi za   kimtambuka. Alisema moja ya sababu zinazoidhofisha michezo Mpwapwa baadhi ya viongozi wa vyama na vilabu kuto kufuata katiba zao   hivyo kupelekea migogoro ndani