WALIMU MPWAPWA WAASWA KUTO KUKOPA MIKOPO YA KUWAZALILISHA.




Kaimu ofisa Elimu  sekondari  wilya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bi Frola Mkwama amewataka walimu kijishughulisha na miradi midogo midogo ya kujiongezea kipato kuliko kujiingiza kwenye mikopo ya watu binafsi  ili kuepuka fedheha zinazo wapata pindi washidwapo kulipa.
Bi Mkwama aliyasema hayo juzi katika mkutano mkuu wa kumi na tisa wa chama cha kuweka na kukopa cha Mpwapwa Teachers Saccos iliofanyika katika ukumbi wa CCM mjini hapa.
Bi Mkwama alisema siku hizi kumeibuka maduka mengi yanayo kopesha  na hivyo walimu   wengi wamejikuta wakidaiwa kadi za Benk na namba za siri kitu kinacho  sababisha walimu wengi kujikuta wakiishi maisha magumu.
Aidha Bi Mkwama  alisema “kwa mwalimu kuobwa kadi na namba ya siri ni kinyume na sheria na privace ya mtu lakini pia haya maduka yanayo kopesha sijui kama yamesajiliwa kama tasisi za kukopesha bali yamesajiliwa kama maduka ya kuuza bidhaa hivyo hata watu wa biashara yachunguze maduka hayo.
Pia alisema hata riba ya  maduka hayo iko juu sana kiasi kwamba yanamuuza sana mkopaji  alisema ili kuweza kuondokana na hilo walimu lazima kujishughulisha na miradi mingine ya kiamaendeleo kama ufugaji biashara ndogondogo ,kwa lengo la kuepukana na mikopo ambayo si rafiki kwao.
 
Kwa upade wake Mwenyekiti wa Chama hicho Bwana Piniel Loilole kwa mwaka 2017 jumla ya shilingi mlion 99,940,000/= zilitolewa na chama  hicho kwa wanachama 88 kwa kipindi cha  januari –December 2017kama mikopo ya kawaida na shilingi milioni 8,910,000 kama mikopo ya dharula.
Loilole alisema kuwa wameamua kutoa mikopo hiyo  ili kuweza kuboresha ustawi wa mwalimu na kuweza  kujiinua kiuchumi na kimaendeleo  kwa lengo la kuodoka kwenye kipato cha chini na kufikia kipato cha kati ambaocho kitaweza kumsaidia mwalimu, kuweza kujenga nyumba bora ,kusomesha na kuwekeza kwenye miradi mbalimbali kama ya kilimo,  na ufugaji. 
Kwa upande wake meneja  wa Saccos hiyo Joakimu Mokiwa alisema kuwa  mikopo  hiyo italeta mabadiliko ya mwanachama  mmommoja   na kukuza  uchumi kwa kaya na  taifa zima.
Pia iliongeza kuwa  pamoja  na kuwezesha wanachama  wake alisema kuna changamoto kubwa   iliyowakabiri kwa mwaka2017 ni baadhi ya watumishi waliogundulika kuwa na vyeti feki  kusimammishwa kazi na hivyo kupelekea chama hicho kupata hasara ya  jumla ya shilingi milion 6,789,6650/=
Hata hivyo alisema  mwajiri kuchelewesha makato ya walimu hao kuingia  chamani na kusabibisha mzunguko wa fedha chamani kusuasua katika uendelevu wake.
 Aliongeza kuwa  walimu lazima waachane   na tabia ya kuchukua mikopo  na kufanyia malengo ambayo hayakuombewa kwenye  mkopo aliwataka kukopa kwa busara na kulipa kwa wakati. 
Pia  Mmoja wa wanachama wa Sassos hivyo mwalimu Neema Mbise alisema wanajikuta  wakijiingiza kwenye maduka ya wakopeshaji yasiyo sajiliwa kutoka na mchakato wa Saccos hiyo kuwa mrefu zaidi hivyo ameuomba uongozi wa saccos hiyo kuweza  kupunguza masharti ya mkopo ili mwalimu anifaike na fedha yake.



Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.