MIMBA ZIMEKUWA KIKWAZO CHA ELIMU MPWAPWA.

Baadhi wa Wadau akisikiliza mjadala wa Elimu  wilayani Mpwapwa.



MKUU  wa mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahaenge amesema nchi zote zinazoendelea  zinatakiwa kuwekeza kwenye Elimu ili kuweza kufikia katika nchi zilizo endelea.
Dkt Mahenge alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akifungua mkuno wa wadau wa elimu wilayani Mpwapwa uliofanyika katika chuo cha ualimu mjini hapa.
Mahenge alisema nchi zote zilizoendelea  ziliwekeza nguvu kubwa katika elimu  hadi kufikia maendeleo zinazojivunia kwa sasa  na kuwa na rasilimali watu wengi  na wazalishaji tofauti na nchi zinazoendelea  kundi kubwa limekuwa si la kuzalisha  na hivyo kubaki kama obwe kubwa la kiuchumi.

Dkt Mahenge alisema kuwa “tunaweza kutoka katika nchi zinazoendelea na kufikia nchi zilizo endelea  kwa kuwekeza sana sana katika elimu  tusione nchi zilizoendelea ziko mbali waliwekeza san asana kwenye elimu  ndugu zangu hatuwezi kufika popote tukiendelea kufanya vibaya  katika elimu lazima tuwandae rasilimali  watu ambao watakuwa wazalishaji katika kilimo,huduma za jamii nk”aliongea Dkt Mahenge.
Katika mjadala huo ulioandalia na halmasahauri ya wilaya yampwapwa ikiwa na lengo la kutadhimini  kubaini change moto, kupanga mikakati  na ya  kuinua elimu katika  wilaya hiyo  ambayo  zaidi ya miaka mitatu mfululizo imekuwa ikifanya vibaya  katika matokeo ya darasa la saba  na kidato cha nne.
Kwa upande wake  Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir Shekimweri  alisema tataizo la mimba mashuleni limekuwa kikwazo kikubwa cha watoto wa kike kuto fikia ndoto zao  na kuachishwa masomo kabla ya  kuhitimu darasa la saba au kidato cha nne.
Shakimweri alisema kwa mwaka 2017 jumla ya wanafunzi 69 walilipotiwa  ujauzito  wakiwa shueni na hivyo kuwapelekea kuachishwa masomo kwa mujibu wa sera ya elimu na sheria ya elimu ya mwaka 2016.
Mkuu wa wilaya hiyo amewaomba wadau wa elimu wilaya hapo kuweza kuchunguza kwa mapana na kubaini chanzo cha mimba mashuleni ili kuweza kuokoa kikazi cha wasichana ambao hufifisha ndoto zao  kabla ya muda.
Ofisa Elimu Msingi wilayani hapa  Bi Mery Chakupewa alisema kwa mwaka 2017 iliweza kushika nafasi ya pili kimkoa  ambayo ilifaulu kwa ufaulu wa asilimi 63.68 ambayo kitaifa ilishika nafasi ya 112.
Bi Chakupewa  alisema  kuwa pamoja na kufanya vizuri katika mtihani wa Darasa la  saba alisema wilaya hiyo inakabiliwa na chanagamoto kadhaa kama uhaba wa vyumba vya madarasa,upungufu wa madawati, pamoja na miundo mbinu  hafifu kwa baadhi ya  maeneo kunako pelekea baadhi ya walimu kukimbia maeneo hayo au kuacha kazi kabisa.
Akitaja shule 10 zilizofany vizuri kwa mtihani kuwa ni shule ya msingi Mtejeta,Vighawe,Kikombo,,Pwaga,Mangangu, Mbunga,Kisisi,Mpwapwa,Kizi na Isighu. Shule zilizo fanya vibaya kumi za mwisho alisema kuwa ni shule ya msingi, Makutupa ,Nzugilo,Kilambo,Igoji Kusini,Idaho,Lufu,Msanga mbuya na Gomuhungile ,


Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.