MVUA ZASABABISHA MADHARA MPWAPWA




 Mvua vua  zinazoendelea kunyesha   hapa wilayani  Mpwapwa mkoani Dodoma kunatishia baadhi     makazi  ya watu  wa  mtaa wa National housing , Majengo na Hazina na vighawe ziko hatarini kusobwa na  maji  kama  hakuna jitihada za makusudi hazitachukuliwa ili kuweza kunusuru  makazi ya watu hao.
 Makazi ya watu binafsi ambazo tayari zimesha sobwa upande ni  ni  baa na nyumba za wageni ya Central , Hapeq pamoja na shule ya na kituo cha kulelea watoto cha The Hiral  kinachomilikiwa na Mwalimu Gisela Kapinga.
 Mvua hizo  ambazo zimekuwa  zikiumiza vichwa  vya viongozi  hapa wilayani  juu ya kazi  ya kuyanusuru  makazi hayo na muindo mbinu  ya tasisi hizo ambazo zilitumia pesa  nyingi katika kuwekeza  na ukamilifu wake wa tasisi hizo.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir Shekimweri     alisema  ofisi yake  kwa kuishirikiana na ofisi ya Tanroad Mkoa  wamefanya  tadhimi  ya awali  ya kuweza  kujua ghalama zitakazo weza kutumika kuayanusuru miundo mbinu  hiyo makazi hayo pamoja na tasisi hizo.
 Shemweri  alisema  pindi watakapo kamilisha kufanya tadhimini wataoa  taarifa kwa kina jumla ya hasara iliweza kusababishwa na mvua zinaendelea kunyesha. 
 Aidha Shakimwei amewataka watu wote wanaoishi katika  mazingira hatarishi kuhama kabla mvua hajaleta madhara makubwa alisema  makazi ya watu waishiokatika mazingira hatarishi hazina  vighawe  na mjimpya yako hatarini zaidi na  watu wasipo chukua tahadhari  mapema hayo yanaweza kusababisha maafa.
Mmmoja wa waaadhilika wa korongo hilo bwana Pankrias Kapinga alisema kuwa  mvua hizo zinatishia kusomba  nyumba yake pia ameiomba serikali kuweza kulinyoshea korongo njia yake ya awali  ili kupunguza maafa yatakayo weza ujitokeza.
Ofisa  afya na mazingira wa wilaya hiyo Bwana Teodory Mlokozi  alisema kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira uliofanywa na  watu katika milima ya kibodyani  kutokana  za shughuli za kibinadamu zimepelekea  maji kuporomoka kutoka katika  milima hiyo kwa   msukomo mkubwa na kusababisha  maji kupasua njia zingine na kuingia katika makazi ya watu.
Mlokozi pia  alisema mabadiliko ya tabia ya nchi  na uharibifu wa mazingira  unaondelea katika  wilaya ya Mpwapwa  umekuwa ni chanzo cha  korongo hilo  kuzidi kuendelea  kuongezeka mwaka hadi mwaka.
Maje  alisema kuwa halmashauri hiyo inakabiliwa na chanagamoto kubwa ya kukosa pesa ya kukabiliana na shughuli hizo  hivyo amewaomba  wadau  kushirikiana  na halamashauri  hiyo kuweza kunusuru  maafa yanayoweza kujitokeza    kipindi hiki cha mvua.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.