KOROSHO MKOMBOZI WA UCHUMI KWA WAKULIMA MPWAPWA

Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabiri Shekimweri akikagua kitalu cha Miche ya Korosho.





SERIKALI Wilayani  Mpwapwa  mkoani Dodoma yawapa changamoto  wanaufaika wa  wa Mpango wa kaya maskini  TASAF  kuacha kutegemea fedha za ruzuku yawataka kujikita katika  kilimo cha Korosho  ili kuwa na uchumi endelevu.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri   juzi alipotembelea miradi uoteshwaji wa miti na vitalu vya korosho  ya  wanufaika  wa Mpango wa  katika vijiji vya  Idilo,Gulwe,Kingiti na Iyenge.
Shekimweri alisema  wao kama serikali lazima wawasaidie wanafaika wa mpango huo kuweza kuwa na  uchumi endelevu kwa kujikita katika ulimaji wa zao la korosho ambalo ndani ya miaka mitatu linaweza kubadilisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na kaya kwa ujumla kuliko kutegemea  fedha hizo za  ruzuku  ya kila mwezi ambazo zitamsaidia  kupunguza  changamoto zake lakini si kuyamaliza.
“Sasa mpango huu wa kila mnufaika kulima heka mbili za  zao la korosho zitasaidia sana   wanufaika   kuwa na uchumi endelevu hata kama  mradi utakapo isha,kama serikali tunaamini mlegwa huyu akilima korosho  ndani ya miaka mitatu huyo mtu si yule ambae alikuwa anategemea  fedha za ruzuku uchumi wake lazima ubadilike” aliongea  Shekimweri.

 Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa akifafanua baadhi ya madini yanayo patikana katika Bibo la korosho kuwa ni vitamin c kwa wingi.

“Kwa  mfano sasa  mtu anaepokea  kiasi kidogo sana ni shiringi elfu ishirini  lakini akilima korosho korosho heka mbili tu ana uhakika wa kupata kiasi cha shilingi milioni nae kila mwaka   sasa hapo si wote tutakuwa matajiri tutakuza uchumi wa kaya uchumi  jamii na wilaya kwa ujumla  inawaomba wote tujiingize katika kilimo hiki ambacho kitaleta mapinduzi makubwa sana ya  kiuchumi na mazingira ndani ya wilaya ya Mpwapwa” aliongea Zaidi  Shekimweri.
Aidha mku wa wilaya hiyo  ametumia Fursa kuwakanya wale wanao pokea fedha za Tasaf na kuzitumia  nje ya Mpango  kuwa lazima wazingatie masharti  mpango  huo ili ziwanufaishe  kwa kiwango cha juu ili pindi mpango utakapo isha waweze kupima   matokeo ya mradi huo.
Kwa upande wake mratibu wa Tassaf  Wilaya ya Mpwapwa  bwana Paskali Symlis alisema kuwa Mpango huo  wa kunusuru kaya  Maskani  tangu uanzishwe mwaka 2014  kwenye vijiji  57  kati ya vijiji113 vya  wilaya  ya Mpwapwa  ambapo unanufaisha  kaya 5990.
Bwana Jeremia  alisema hadi kufikia  mwezi Desemba mwaka huu mpango huo umeweza  kutoa ruzuku kwa awamu 20  na umla cha kiasi cha shilingi billion  4,774,383,500/= zilitolewa  kwa walegwa kama  ruzuku ya msingi  na  malipo kwa ajili ya ajila za muda.
Pia Bwana Jeremia alisema  ili kuhakikisha kuwa walegwa wanakuwa na kipato cha  uhakika  na endelevu  halmasahauri kwa kushirikiana  na walegwa  kupitia  mpango wa umeanzisha kilimo cha korosho  kwa vijiji  22 vyenye  walegwa 2396.
Alisema katika mpango huo wanategemea kulima heka 4792 za korosho  ambazo zitaweza kuleta mabadiliko ya kijani pamoja na uchumi wa kaya na jamii kwa ujumla.
Mmoja wa wanufaika wa Mpango  wa Mpango huo BiJaneth Yeremia alisema pamoja na mpango huo  kuwalipa baadhi ya walegwa katika ajira za muda lakini walegwa 12 wa kijiji cha kingiti hawakulipwa   malipo yao  japo kuwa walifanya kazi.
Pia  miongoni mwa wanufaika wengine ambae hakauta jina lake kuandikwa alisema  kuna baadhi ya watendaji na baadhi ya wasimamizi wa mpango huo CMT wamekuwa wakiwakata fedha zao za ruzuku  pasipo kuwa na maelezo ya kutosheleza  kitu alicho kisema kuwa kinaonyesha mianya ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.