VITA YA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NI ZAIDI YA UGAIDI.


Hii ni miongoni mwa nyumba za mwanzo am[o baba wa taifa marehemu Nyererealikuwaakifanyia mikutano yake humo ikombioni kusomwa na maji kutokana na uharibifu wa maxingira.
VITA YA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NI ZAIDI UGAIDI.




 MAZINGIRA ni uhai,Mazingira ni vitu vyote vinavyo tuzunguka vyenye na uhai na visivyo na uhai, vitu vyenye uhai ni  mimea na wanyama na visivyo uhai  ni pamoja na hewa  ardhi na  maji, mazigira yanahusisha vitu vyote kuendelea na kuwepo kwa viumbe vingine.
 Maisha ya viumbe vilivyopo na vijavyo utegemea   mawasiliano mazuri kati ya mazingira  watu na,uhai, uhuru na usatawi wa taifa letu la sasa hutegemea sana maisha yanayo tuzunguka, leo hii uharibifu wa mazingira umekuwa ni  nitishio kubwa la uhai wa binadamu na mataifa mbalimbai ulimwenguni.
Mabadiliko ya tabia ya nchi ni tishio la usalama wa maisha kama ilivyo kwa ugaidi  na vita,  sote tumekuwa mashaidi njisi tunavyoshuhudia njisi mvua zimeendelea kushuka na kuto kuwa za kutabilika  siku hadi  siku ,joto limezidi kuongezeka  ukubwa  wake kutokana   na uharibifu wa mazingira katika hali hiyo   ndicho miongoni mwa sababu kubwa za migogoro ya ardhi  kati ya wafugaji na wakulima ,uhaba wa chakula, na umaskini iwapo hatua za makusudi za  uhifadhi wa mazingira  hazitachukuliwa vya kutosha.
Mazingira ni afya  yetu mazingira ni uhai wetu na mazingira ni uhuru wetu.
Katika nchi yetu ya Tanzania misitu alianza kuhifadhiwa tangu enzi za ukoloni mwaka 1859 wakati wa enzi za wajerumani,juhudi hizo ziliendelezwa na waingeleza mala baada ya  vita kuu ya dunia  mwaka 1914-1918 baadhi ya misitu ilianza kutengwa na kuhifadhiwa kisheria mwaka 1930 -1952.
Kimsingi masuala ya  uhifadhi ilipewa kipaumbele sana  wakati wa serikali ya waingeleza ,wakati sera ya kwanza ya misitu iliwekwa mwaka 1953 ,ilifanyiwa malejeo mwaka 1957 ambapo ilitumika hadi mwaka 1977, ambapo ndiyo iliopo hadi sasa, 1998 Sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2002 ilitayarishwa mahususi kwa  lengo la kuhifadhi  na kuendeleza misitu kisheria.
Misitu ni mali asili inayo hifadhi maji kwa kiwango kikubwa sana ikumbukwe kuwa  mizizi ya miti husababisha nyufa katika ardhi na kutokea kwa chemchem nyingi za asili.
Uharibifu wa mazingira na misitu una madhara makubwa kwa uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja uihifadhi wa mazingira afya na mazingira pia ni sehemu ya kawaida kwa maisha ya mwanadamu popote alipo.
Wilayani Mpwapwa, yako maeneo ambayo kihistoria yalikuwa ni sehemu tegemeo kubwa kwa maisha ya watu ikiwa ni pamoja na Maendeleo yao. Upo ukweli usiopingika kuwa Mpwapwa ilikuwa ikiongoza kwa kulisha chakula Mkoa Mzima wa Dodoma pamoja na mikoa jirani, kabla ya kuharibika kwa mazingira katika wilaya hiyo.

Hivi sasa imebaki historia kwani maeneo mengi yanaonekana kuharibika vibaya huku mamlaka husika zikiwa zinaumiza kichwa juu ya namna ya kukabiliana na uharibifu huo.

Kijiji cha Mima,Lwihomelo,na kijiji cha Kibodyani ni mfano wa maeneo ambayo yalikuwa na mazingira mazuri lakini kwa sasa ni miongoni mwa Vijiji vya mfano mbaya kwani Milima ya kijiji hicho hivi sasa imekuwa ni vipala.
Wananchi wamevamia maeneo ya milima na kuchoma moto,  kulima katikati ya msitu lakini bado watendaji wa kata, vijiji , na wanasiasa wanaendelea kupata kigugumizi njisi ya kuwachukulia hatua waharifu wa mazingira hayo tunajiuliza ni kuto kuelewa sheria au ndo ile hali ya kukingiana vifua.

Moja wapo ya Eneo  lililofyekwa katika mlima Mkanana kata ya Berege Wilayani Mpwapwa.
Bila shaka wanashindwa kufanya hivyo kutokana na sababu zao binafsi ambazo wanazijua wao, ama ni kwa makusudi au hata kuaminishwa kuwa labda na wao ni miongoni mwa watu hao wanaoharibu mazingira wao wakishirikiana kwa uzembe.

Hata hivyo si vema kuhukumu kwa upande mmoja, lakini inafaa kutazamwa kwa mapana na marefu ili kubaini ni wapi panapohitaji kuangaliwa kwa macho mawili.

Salum Kabanda ni meneja wa  wakala wa kuhifadhi misitu ya asili wilayani Mpwapwa ambaye anatahadharisha kuwa kama juhudi za makusudi hazitachukuliwa ni wazi kuwa wilaya hiyo muda mfupi ujao itakuwa ni jangwa.“Achilia mbali kugeuka jangwa, lakini katika kipindi cha miaka 10 ijayo hakutakuwa na maji katika wilaya hii kama mnavyoona hilo halifichiki nduguzangu,’’anasema  Salum.

Kabanda  anasema kuwa ifikapo mwaka 2027 hakutakuwa na maisha katika wilaya hiyo na kwamba viumbe hai wote wataishi kwa taabu  na huenda vifo vikatawala kwani juhudi za kuharibu mazingira ni kubwa kulikojuhudi za kuyalinda.

Mtaalamu huyo anaonya kuwa hakuna sababu za aina yoyote kwa binadamu kupigalamli juu ya kwa nini maisha yanakuwa ni magumu wilayani Mpwapwa bali ni vema kuangalia wapi waliko jikwaa.


Kauli ya mtaalamu huyo zinamfanya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa JabirShekimweri kuapa kuwa atakufa na waharibu mazingira.

Mkuu huyo ambae tangu ateuliwe kuwa mkuu wa wilaya  mwaka mmoja uliopita  anasema hana kitu kingine ambacho anasema kujivunia isipokuwa ni namna ambavyo atafanikisha mapambano na waharibifu mazingira Mpwapwa.

Anasema  ili kufikia malengo lazima waanze kupanda miti katika  tasisi za serikali kama shule za msingi,sekondari na tasisi zote za serikali pia ataongoza mashambulizi ya watu ambao watakuwa ni wakata miti na kuharibu vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kilimo cha milimani.“Nitatumia hata dola kwa ajili ya kuongoza mashambulizi ya mapambano hayo, siwezi kulala na sikubali kushindwa hata siku moja maana inauma kweli  ambavyo Mpwapwa imeharibika,’’anasema Shekimweri.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmasahauri ya wilayani Mpwapwa  Mohamed Maje anasema kuwa  kuna watu wengi walio vamia  maeneo ya muhimu ikiwemo hifadhi ya misitu ya asili  ijulikanayo kama milima ya safu za milima ya TAO za mashariki.

Maje anasema Milima hiyo ambayo inapatikana katika Kata za Lufu na Lufusi ni milima muhimu sana kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sahihi za asili ya Mpwapwa tangu enzi za ukoloni.
Alisema kuwa uvamizi katika maeneo hayo ni mkubwa na ambao usingepaswa kuvumiliwa hata siku moja lakini akashangazwa kuona viongozi walioko katika maeneo hayo husika  kuendelea kuwafumbia macho.
Maje  anabainsisha madhara yatakayojitokeza kwa siku za usoni kuwa ni zaidi ya watu 300,000 kukosa chakula na kushuka kwa uchumi wa familia hizo kutokana na kukauka  kwa vyanzo vya maji katika milima hiyo.
Mbali na kukosekana kwa maji kwa wakazi wa maeneo hayo.
Pia alisema lazima waunganishe Nguvu kati ya Wilaya za Kilosa na Iringa Vijijini  katika harakati za kupambana na uharibifu wa mazingira ambapo madhara yake yanazigusa wilaya hizo tatu.

  Maje alidai kuwa  kutokana na uharibifu huo   Wilaya za Mpwapwa, Kilosa,Iringa Vijijini na Chamwino zinaweza kukwama katika mpango wa serikali wa umwagiliaji.

Milima ya Tao za Mashariki  Wilayani Mpwapwa  ndicho chanzo kikubwa cha maji  ambayo hutumika katika  shughuli za  za kilimo cha umwagiliaji  wa zao la  mpunga katika bonde la Lumuma.

Bonde hilo ni maarufu kwa wananchi wa wilaya za Mpwapwa na Kilosa ambalo linalimwa zaidi Mpunga,vitunguu na  mahindi na maharagwe.

 Kutokna na Uvamizi huo katika milima hiyo, kumepelekea bonde la Lumuma kupungua kwa maji  na hivyo wananchi wanaoishi kwa kutegemea bonde hilo hivi sasa wanaishi maisha ya ‘chungu moto’Kutokana na hali hiyo pia alisema itaadhiri mapato ya halmashauri.

MWISHO

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.