SERIKALI YAJIPANGA KUTOA CHANJO YA SARATANI

Naibu waziri wa afya mandeleo ya jamii, jinsia, wazee, na watoto Dr. Faustine Ndungulile amesema kuwa serikali inatarajia kuanza kutoa chanjo ya kujikinga na saratani ya matiti pamoja na saratani ya shingi ya kizazi kwa mabinti wenye umri wa miaka 14 mapema mwezi April mwaka huu.

Kwa mujibu wa Takwimu za shirika la afya duniani ya mwaka 2012 zinaonyesha kuwa 80 ya saratani ya mlango wa kizaza zinatokea katika nchi zinazoendeleo,ukilinganisha na nchi nyingine za afrika mashariki Tanzania inaongoza kwa kuwa na wagonjwa 50.9 kwa kila wanawake 100,000 lakini pia tunaongoza kwa kuwa na vifo 37.5 kwa kika wanawake 100,000.

Akizungumza leo mjini hapa wakati akizindua kampeni ya kupima saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti Dr. Ndungulile alisema kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo serikali imeona ni vyema kuanza kutoa chanjo wa ugonjwa huo.

Amesema kuwa watarajia ndani ya mwaka huu kutoa chanjo kwa mabinti wapata 6,16,734  nchi nzima.


Amesema kuwa wao kama serikali baada ya kuona utafiti huo wameona wajielekeze kwenye kutoa chanjo hiyo ili kuwalinda mabinti nakupunguza uwezekano wa wao kupata saratani ya mlango wa kizazi huku akisema kuwa saratani hizo zinaweza kuepukika.



Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Binilith Mahenge akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi amesema kuwa maamuzi ya kutoa kampeni hiyo ni sahihi ili kufanya wananchi tumia fursa hiyo kupima afya zao na badae kupataiwa matibabu.


katika chanjo hiyo wamelengwa mabinti ambao wapo mashuleni hivyo wazizi wanaombwa pindi wapatapo taarifa hizo kutoka kwa waalimu wa shule watoe shirikiano kwani maamuzi ya serikali ni mema kwa mabini hao.


Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.