ZAIDI YA BILIONI 15 ZINAHITAJIKA KUKAMILISHA JENGO LA RC DODOMA.

ZAIDI ya Sh.Bilioni 15 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa jengo la Mkuu wa mkoa wa Dodoma ambalo linatarajiwa kuwa ni ofisi ya Rais na Makamu wa Rais ambapo ujenzi huo kwa sasa umefikia asilimia 56.

Akizungumza wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa dodoma Dk.Binilith Mahenge wakati wa ukaguzi ujenzi wa jengo hilo Msanifu wa majengo wa kampuni ya (CRJE) Peter Kibushi amesema fedha hizo sh. bil 15.9 za awamu ya tano pindi zitakapotolewa zitakamilisha ujenzi huo.

Akisoma taarifa ya ujenzi huo, Msanifu huyo amesema ujenzi wa jengo hilo ulianza Juni 2009 na utagharimu zaidi ya Sh.Bilioni 25 ambapo hadi sasa fedha zilizotolewa ni takribani Sh.Bilioni 12.



Naye Mhandisi Mshauri wa ujenzi huo, Titus Tesha amesema wamelazimika kujenga kwa awamu kutokana na mtiririko wa fedha kuwa mdogo na hivyo kupanga kazi kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.

Akizungumzia kuhusu utoaji wa fedha kwa ajili ya jengo hilo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Deogratias Yinza amesema katika mwaka wa fedha 2017/18 zimetengwa Sh.Bilioni 2.3 kwa ajili ya jengo hilo.



Dk.Mahenge akizungumza mara baada ya kukagua jengo hilo, amesema ameridhishwa na ujenzi unaoendelea na kuipongeza serikali kwa mradi huo mkubwa.

I
Ujenzi huo wa jengo hilo ulianza rasmi june 2009 kwa kutumia bajeti ya mwaka wa fedha 2009/2010 na ulikadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi billion 15.2 huku ukitakiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu lakini hali imekuwa tofauti kutokana na mtiririko wa fedha usioridhisha ambao umesababisha ujenzi huo kuchelewa kukamilika wa muda uliotakiwa.



Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.