MAAFISA MAENDELEO TIMIZENI WAJIBU WENU-WAZIRI WA AFYA.



WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii wote kutekeleza wajibu wao wa msingi kwa kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya vitendo vya ukatili wakiwa shule na nje ya shule.

Taarifa ya utafiti wa hali ya afya ya uzazi ,mtoto na malaria ya mwaka 2015/2016 inaonyesha kuwa asilimia 27 ya watoto wakike wanapata mimba wakiwa na umri chini ya umri wa miaka 18..

Tatizo hili lipo zaidi mikoa ya Katavi (asilimia 45),Tabora (asilimia 43),Dodoma (asilimia 39), Morogoro (asilimia 39) na mkoa wa mara (asilimia 37)

Akizungumza leo mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa 12 wa sekta ya maendeleo ya jamii Waziri Ummy amesema kuwa kupitia mkutano huo maafisa maendeleo ya jamii amesema kuwa kupitia mkutano huo maafisa maendeleo ya majii wanatakiwa wanatoka na mikakati madhubuti ya kudhibiti vitendo vya ukatili katika jamii.



Naye Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga amesema kuwa katika awamu ya sasa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii wana wajibu wa kuelimisha na kuhamsha ari ya wananchi kufanya kazi za uzalishaji.



Kwa upande wake mkurugenzi wa maendeleo ya jamii tika wizara ya afya maedeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, idara kuu ya maendeleo ya jamii Patrick Golwike amesema kuwa wao kama maafsa maendeleo ya jamii wanatakiwa kutambua majukumu yao.


Takwimu za elimu kwenye shule za msingi kwanzia mwaka 2011 hadi 2015 zinaonyesha kuwa wasichana elfu 39,243 waliacha shule kutokana na sababu mbalimbali na wasichana elfu 3,806 walikatishwa masomo yao kwasababu ya mimba.

Kutokana na hayo maafisa maendeleo ya jamii anawataka kufuatilia mwenendo wa taarifa zitakazotolewa na wakuu wa shule ili kubaini ukubwa wa tatizo katika halmashauri kwa lengo la kubuni na kupanga mbinu za kukabiliana na tatizo hilo kwa watoto walio shuleni.

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.