MKURUGENZI MPWAPWA AITAKA JAMII KUHAMASIKA KATIKA MAENDELEO.




SHULE ya Msingi Mngangu  wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma inakabiliwa  uhaba wa matundu ya vyoo  hali hiyo inapelekea  kuwapo kwa mazingira magumu kwa walimu na wanafunzi kwa  ya kujifunzia na kusomea.

Mwenyekiti wa kijiji  hicho  bwana   Sospiter  Nyaombo  amesema kufutia hali hiyo bwana jamii wakajihamasisha na kujenga matundu ya  kumi mbili ya vyoo vitakavyo ondoa adha   kwa wanafunzi kulundikana vyooni wakati wa mapumziko .

Bwana Nyaombo amesema “mpaka sasa kupitia nguvu za wananchi  tumesha  jenga matundu kumi na mbili ya   vyoo ambayo yatapunguza adha ya matundu ya vyoo  shuleni hapo lakini kwa kutambua majukumu yetu tumesha chukua hatua ya kuwaondolea kadhia hiyo watoto wetu ili wasome katika mazingira rafiki na hatimae kukuza kiwango cha ufaulu shuleni hapa.”aliongea Bwana Nyaombo.

Aidha mwenyekiti wa  kamti ya shule hiyo bwana  Sajilo Nuhu amesema shule hiyo yenye wanafunzi  461 lakini ina matundundu  nane tu ya vyoo yanasababisha mlindikano wa wanafunzi vyooni  lakini pia kutishia kwa magojwa ya mlipuko hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mvua za vuli.

Bwana Sajilo amesema pia shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa,madawati nasamani zingine za ofisini kwa walimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa bwana Mohamed Maje amesema wao kama serikali wameshatoa bati thelathini na mifuko  30 ya sementi kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi wa vyoo hivyo .

Bwana Maje   amewapongeza wanachi wa kijiji cha Mangangu  kwa kuhamasika kuondoa  changamoto ya vyoo katika shule yao na aliwataka wananchi wa vijiji vingine kuweza kuiga mfano wa kijiji hicho katika  kutatua changamoto za lkimaendeleo kwa kutumia nguvu kazi kazi walizonazo na rasilimali zinazo wazunguka.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.