WAZIRI ATAKA CHANGAMOTO ZA MAJI KUISHA VIJIJINI



Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi Izack Kamwelwe amesema katika kukabiliana na kero ya upatikanaji wa huduma ya maji wilayani Kongwa mkoani Dodoma serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni 600 kwa ajili ya miradi ya maji wilayamo hiyo.

Wilaya ya Kongwa ni miongoni mwa wilaya kongwe zilizopo makao makuu ya nchi Dodoma licha ya ukongwe wa wilaya hiyo bado wananchi wake wanateseka kutafuta huduma ya maji na kulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo muhimu.

Hali hiyo inamlazimu Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Izack Kamwelwe anafanya ziara wilayani humo na kutoa matumaini mapya kwa wananchi katika kutatua tatizo hilo sugu na kuahidi serikali itamaliza tatizo la upatikanaji wa huduma hiyo ndani ya muda mfupi.


Mhandisi Izack Kamwelwe Waziri wa maji na umwagiliaji
Deo Ndejembi ni mkuu wa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara amesema kuwa atahakikisha anasimamia ujenzi wa miradi ya maji ili wananchi waweze kupata maji safi na salama


Deo Ndejembi mkuu wa wilaya ya Kongwa
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Chiwe wilayani Kongwa mkoani Dodoma wamesema kuwa wamekuwa wakiteseka kusaka huduma ya maji umbali mrefu na kuiomba serikali kuhakikisha inawapatia huduma hiyo


Zaidi ya miradi 1810 ndiyo ilipangwa kutekelezwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016­/2017 na kati ya miradi hiyo ni 1435 ndiyo imetengenezwa hivyo bado jitihada zinahitajika katika kuumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya masji

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.