KOROSHO ITAGEUZA UCHUMI WA DODOMA


WAKULIMA  wa Mkoa wa Dodoma wameshauriwa kujikita katika ulimaji wa zao la korosho kwani zao hilo lina faida kubwa kibiashara tofauti na yalivyo mazao mengine.

 Korosho ni moja ya mazao makuu ya biashara nchini. Kwa sasa zao hili hulimwa zaidi mikoa ya Kusini mwa Tanzania, yaani Lindi na Mtwara ikifuatiwa na Mkoa wa Ruvuma, Pwani na Tanga.

Takwimu kutoka Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) zinathibitisha umuhimu wa zao hilo kwa Taifa, ambapo katika msimu wa 2012/13 zao hilo liliiingizia Serikali kiasi cha Sh bilioni 29.5 kutokana na ushuru wa usafirishaji wa korosho ghafi nje ya nchi.


Akizungumza wakati wa ziara yake katika baadhi ya wilaya za mkoa huo  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr.Binilith Mahenge ameeleza kuwa utafiti umefanywa na kubaini ardhi ya Dodoma inafaa kwa uzalishaji wa zao hilo.



Akitoa taarifa ya wilaya kwa Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa wilaya ya Kondoa Sezaria Makota amesema wilaya yake imeanza kuwa na mkakati wa zao la korosho kama zao la biashara na hadi sasa wameshapokea mbengu ya zao hilo kutoka katika Bodi ya Korosho.

Aidha Dr.Mahenge amepingana na wanaodai kuwa Mkoa wa Dodoma ni kame na kusisitiza kuwa ni lazima wakulima walime mazao yanayo endana na hali ya hewa ya mkoa huu.


Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.