UKATILI WA KINJISIA UWEKEWE MKAKATI MADHUBUTI



SERIKALI ya Mkoa wa Dodoma imewataka wakurugenzi wa wilaya zote ndani ya mkoa ,sekretarieti ya mkoa pamoja na watendaji wengine katika ngazi zote kutekeleza kwa vitendo majukumu yote waliyopangiwa kwa mujibu wa mpango wa kitaifa wa kutokomeza  ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Maagizo hayo yametolewa hii leo na kaimu mkuuwa mkoa wa dodoma ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamoga wakati wa ufunzguzi wa maadimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili dhidi ya wananwake na watoto ambapo mbali na hayo pia ametoa magizo kwa maafisa maendeleo na ustawi wa jamii huku akisistiza kuwa maagizo hayo yatafatiliwa kwa kadri itakavyotakiwa.


Aidha pia Nyamoga amesema wananchi wengi wamekuwa wakiwatoa malalamiko  watendaji wa vijiji na kata kujihusiha na vitendo vya rushwa jambo ambalo linadidimiza jitihada za kutokomeza ukatili dhidi ya wananwake na watoto jambo ambalo kwa mkoa wa dodoma halikubaliki.


Kwa upande wake mwakilishi wa katibu mkuu  wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto idara kuu ya maendeleo ya jamii,mkurugenzi wa maendeleo ya jamii  Patrick Golwike amesema  kwa kutambua ukubwa wa tatizo hilo la ukatili dhidi ya wanawake na watoto serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika kukomesha tatizo hilo.


Aidha naye  mwakilishi  kutoka mtandao wa kutokomeza ukatili wa kijinsia (MKUKI) Sarah Mwaga amekuwa na haya ya kusema.

Maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika jijini dar es salaam na kanda ya kati maadhimisho hayo yanafanyika mjini morogoro ambo kimkoa yamefanyika Wilaya ya Dodoma.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.