SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU TAHADHARI ZA MVUA.

SERIKALI imetoa tahadhari ya mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini huku ikielekeza wananchi kutumia fursa chanya za mvua hizo kwa shughuli za maendeleo kama kilimo kwa ajili ya kupanda mazao yanayohitaji maji.

Mbali na kilimo pia wananchi wametakiwa kutumia mvua hizo kuandaa mabwawa na malambo kwa ajili ya uvunaji wa maji .
  
Tahadhari hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera, Bunge, kazi, ajira,vijana na watu wenye ulemavu Stella Alex wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa kamati za usimamizi wa maafa kuanzia ngazi ya kijiji na mtaa zinatakiwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa maafa NO.7 ya mwaka 2015 na kanuni za usimamizi wa maafa za mwaka 2017.


Amesema kuwa septemba 4 mwaka huu Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ilitoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Octoba mpaka disemba mwaka huu kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua na kuonyesha maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kupata mvua za wastani.

Kwa sasa tayari baadhi ya maeneo yaliyotabiriwa kupata mvua nyingi yameanza kupata madhara yalizosababishwa na mafuriko ikiwemo vifo,magonjwa ya milipuko,uharibifu wa mazao mashambani,uharibifu wa mazingira,mali na miundombinu ambapo pia inadaiwa madhara yanayoweza kuongezeka kama hatua stahiki hazitachukuliwa.


Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.