mwakyembe amg,oa bkigogo wa kigogo usafirishaji ATCL


0digg
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe
Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ametengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Paul Chizi na amewasimamisha kazi wakurugenzi wanne kutokana na “ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, ambao umetishia uhai wa shirika hilo muhimu kwa taifa.”Kutokana na hatua hiyo, Dk Mwakyembe amemteua rubani wa siku nyingi katika shirika hilo, Kapteni Lusajo Lazaro kukaimu nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Chizi.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Omary Chambo alisema Dar es Salaam jana kwamba Waziri amefikia uamuzi huo kutokana na taratibu za uteuzi kwa wafanyakazi wa umma kutokufuatwa.
Alisema nafasi aliyopewa Chizi haikutangazwa kama sheria na kanuni zinavyotaka...  “Uteuzi wake haukufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, hivyo kupitia Sheria Na 8 ya mwaka 2002 na kanuni ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2003 Na 17(4), Dk Mwakyembe ametengua uteuzi huo kuanzia jana.”
“Kanuni hii inaeleza bayana kuwa kama mtumishi atakuwa ameteuliwa kwa kukiuka Kifungu cha 17(1 au (3) za Kanuni za Utumishi za mwaka 2003, itakuwa ni mamlaka ya uteuzi wa kutengua uteuzi wa utumishi wake mara moja.”
Kabla ya kuteuliwa na kushika wadhifa huo na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, Chizi aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Community Airline.
Wakurugenzi wanne waliosimamishwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhandisi, John Ringo, Mwanasheria wa ATCL, Amini Mziray, Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Justus Bashara na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Josephat Kagirwa.
Mhandisi Chambo katika taarifa yake kwa umma, alisema kutokana na ukiukwaji huo wa taratibu, itaundwa kamati yenye wajumbe watatu wenye uelewa wa mambo ya fedha na sheria kuchunguza matumizi ya fedha zilizopokewa kuanzia mwanzoni mwa Mei mwaka huu.
Alipoulizwa ni fedha kiasi gani kilichopotea, alisema tu kwa kifupi: “ni fedha nyingi sana kutoka idara mbalimbali.”
Hatua hiyo ya Dk Mwakyembe imekuja siku chache baada ya kuonya kwamba atalifumua Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) ambalo pia lipo chini yake baada ya kuona linasuasua kama ilivyo ATCL.
ATCL lilianza kuwa hoi baada ya kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) mwaka 2002 na baada ya kuvunjika kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATC).
Tayari Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amewahi kuishauri Serikali kuwa vema ingelivunja shirika hilo na kuliunda upya.
CAG katika ripoti yake ya mwaka huu alipendekeza kwamba uongozi uliokuwapo ulishindwa kuonyesha mikakati ya namna gani wangelitoa shirika hilo lilipo na kulipeleka mbele.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
+2 #8 wanakayaya 2012-06-06 12:43
nakupa tano,ila haitoshi washitakiwe kwa kuhujumu uchumi
Quote
 
 
+1 #7 kesmby 2012-06-06 11:17
wakamue timua timua walafi wote tupa selo,tena kama vp tufate sheria ya china kamata fisadi nyonga, mana mijitu mijizi ukiitimua itakwenda idara nyingine tena na kuiba dawa ni kuinyonga tu
Quote
 
 
+1 #6 Ingini ya Timu 2012-06-06 09:52
hongera sana Mh. Dr. mwakyembe sasa watu wataheshimu kodi za walalahoi wanazozifuja, embu liangalie kwa mapana shirika la reli Tazara.
Quote
 
 
+1 #5 jacob kijazi 2012-06-06 09:14
mwanzo mzuri unatutia moyo, usirudi nyuma hata kama baadhi ya watu hawatakubali simamia kwenye haki na ukweli usimuonee mtu. na kama ukithibitika kuwa kuna ubadhilifu wa mali ya umma, please, please, isishie hapo sheria ikamate mkondo wake. mahakama si kwa vibaka tuu na wezi wa kuku hata hao wanaojiita wasomi wanaolipeleka taifa letu kusikotakikana na waonje joto ya jiwe.
Quote
 
 
+1 #4 Doekulu 2012-06-06 09:01
Pongezi kwako muheshimiwa raisi kutupa mtu kama huyu Mwakyembe,natum aini shirika letu la ndege litakuja juu na rasilimali za wa tanzania zitakuwa salama,mawaziri na wa watendaji wote wa serikali tupeni raha jamani.
Quote
 
 
+1 #3 mtumishi 2012-06-06 08:52
Pongezi kwako mzalendo wa kweli muheshimiwa mwakyembe,tukip ata wazalendo wa kweli wa namna hii taifa hili linaweza kupiga hatua kubwa sana
Quote
 
 
+1 #2 Nyaku 2012-06-06 08:32
Mie nampongeza Mh. Waziri kwa hatua aliyoichukua lakin awe makin na anachokifanya kwa mwisho wa siku isije ikawa ni nguvu ya soda
Quote
 
 
+1 #1 lema g 2012-06-06 08:22
tusifanye maamuzi ya harakaharaka kwa kuogopa wabunge
maamuzi mengi yamefanyika bila kufanyiwa tathmini za kutosha na kusababisha matatizo mengine makubwa baadaye.
mfano mzuri wakati mwingine raisi huchlewa kufanya maamuzi sio kwa kushindwa bali kusubiri tathmini za kina zifanyike pmoja na kwamba wakati mwingine hazifanyiki sawa sawa ila ni vizuri zifanyike
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!



7000 symbols left


Banner
Banner
Banner

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.