ASASI ZA KIRAIA ZA LALAMIKIWA KUTO KFIKIA MALENGO.

Na  noel Stephen Mpwapwa
I mebainika kuwa  Asssi za kiraia  nchini  japo kuwa  zimefanya kazi kubwa kwa jamii na  serikali lakini bado hajijafikia malengo yanayo takiwa kutokana na rasilimali zilizo tumika na matokeo yanayo onekana.
  
H ayo yamebainishwa  na  Bwana  AYUBU KUPONA  afisa mipango kitengo cha Sera  na  Maendeleo katika ukumbi wa  Hoteli ya Blue Pearl mjini  Dar –ES-Salaam  alipo kuwa   akifungua  warsha ya  watendaji Wakuu wa AZAKI TANZANIA.

Bwana kupona  alisema kuwa  japo kuwa asasi nyingi  zimefanya kazi   nchini bado  kuna changomoto ya kuyafikia malengo  yaliyo kusudiwa  ingawa pesa nyingi imetumika katika kitengo hicho kitu alicho sema kuwa matokeo haya endani  na kiwango cha rasilimali zilizo tumika .

Aidha alidai kuwa   asasi nyingi nchini bado hazijafanya kazi za kufuatilia  mambo makuu ya  kitaifa  ili kuweza  kuleta  mabadiliko yanayo mgusa mlegwa wa hali ya chini TANZANIA.

Pia alidai kuwa  yapo mabadiliko ambayo yanaonekana  kwa jamii na kuleta matokea  yanayo tia moyo bali alizitaka assi za kiraia  kujitahidi kutumia rasilimali kidogo walizonazo  ili kupunguza malalamiko  ambayo hutokea kutoka kwa wadau na  walegwa pamoja na serikali nchini.

 Akiongea mmoja wa wanawarsha  kutoka katika  kituo cha wasaidizi wa  kisheria IRINGA paralegal  Bwana  Sigfrid Mapunda  alisema kuwa asasi nyingi  nchini zimeshidwa  kusimamia dhima na  dira ya shirika  kitu alicho kisema kuwa  kinashusha utendaji wa shirika na kupelekea kushidwa kuyafikia  matokeo yaliyo kusudiwa.

Pia wanawarsha hao kwa pamoja walidai kuwa  watendaji wengi wa asasi wana uelewa mdogo juu mambo ya uongozi wa asasi kitu walicho kisema kuwakinapelekea  kuwa na migogoro mingi ndani ya  asasi nyingi hapa nchini.

 Kwa upande wake  Bwana STEPHEN LWITIKO mratibu wa mtandao wa mashirika  yasiyo kuwa ya kiserikali  wilayani mpwapwaNGOMNET alidai kuwa udhaifu  miongoni mwa katiba za mashirika kunapelekea  kuwepo kwa  muingiliano wa majukumu kati ya bodi ya ukurugenzi na watendaji wakuu wa Asasi.

Katika Warsha hiyo ambayo ilikuwa ya kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi ndani ya asasi wakuu hao waliweza kuainisha majukumu ya  watendaji wakuu wa asasi ambapo alisema kuwa ni  kubaini Dira, dhima,  na malengo mahususi ya  ASASi.

Mengine  ni kuhakisha kuwa na uongozi wa sheria na  uwajibikaji ndani ya Asasi  na kubaini ,kufuatilia  uwezo wa tasisi  kuhusu huduma  za  program  zake.







Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.