MKUU WA WILAYA AHIDI KUJIUZULU AKISHIDWA KUPAMABANA NA RUSHWA

 Na Noel stphen mpwapwa ..
 MKUU WA WILAYA ya  Mpwapwa bawana  CHRISTOPHER KANGOYE ameahidi  na amesema yuko tayari kujuuzuru ukuu wa wilaya kama  endapo atamkamata mtu yeyote na rushwa  harafu huyo mtu asijukuliwe hatua za kisheria na vyombo vinavyo husika.

 Bwana Kangoye ameyasema hayo  mwishoni  mwa wiki  wilayani mpwapwa alipo kuwa akifungua  mjadala  wa wazi  wa Tasisi ya Kuzuia na kupambana  na Rushwa Wilayani hapo mkoni Dodoma  (PCCB)

 Alisema kuwa yeye amekuja wilayani mpwapwa kwa  ajili ya kuwatumikia wana mpwapwa na  sio kutumikiwa na wana mpwapwa,  hivyo alisema hapendi kusikia  malalamiko ya wanancjhi juu ya  kunyanyaswa na baadhi ya watendaji wa serikali na tasisi zake kwa kuombwa rushwa kwenye haki zao za msingi kama  afya  elimu maji  na utumishi.

Aalisema  kuwa umaskini haiuwezi kuondoka kwa kuendekeza  rushwa na kufichaficha  mambo kwa kulindana kwa baadhi ya watendaji wa serikali pindi   mtu apatikanapo na  tuhuma za rushwa au  ubadhilifu wa mali za serikali.

Kwa upande wake kamanda wa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wilayani hapa  Bwana Maiko Makoba  alisema kuwa kuna tetesi nyingi na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya kulalamikia huduma wapatiwazo kwenye hospitali za  serikali kuwa wananyanyaswa na kuobwa rushwa wakati wa kutaka huduma.


Pia Makoba alisema  kuwa huduma ya afya lazima ipewe kipaumbelekwa wahudumu wa afya  kufanya kazi  kwa  moyo ili  wananchi wanapo patwa na malazi lazima wataenda kutibiwa hivyo kama watendeji wa afya wanaendekeza rushwa wanachi watanyanyasika sana  na kupelekea kuichukia serikali iliyoko madarakani  na kuitolea lugha chafu kitu alichosema kuwa lazima watendaji wa idara hiyo kuzingatia maadili na kanuni za kazi.

Katika mjadala huo wa wazi Bwana makoba aliwataka wanachi kutoa kero zinazojitokeza katika sekta ya afya ili wajirekebishe na  kuweza kutoa huduma bora na  zenye tija kwa jamii  na walipa kodi

Akiongea mmoja wa wachangiaji katika mjadala huo aliye jitambulisha kwa jina la David Thomas alida kuwa  huduma ya bima  ya afya ya jamii haina tija kwa wanyonge; pamoja na kuwa na bima lakina ukienda hosptalini unaandikiwa dawa tatu unapewa moja na zingine unaambiwa ukanunue wakati jana tu gari la MSD limeshusha dawa iankuwaje kanma sio rushwa  ni nini”?alihoji bwana  Thomasi
AIDHA pia  wananchi hao walisema kuwa  wadi ya wazazi huobwa kila mzazi ajifunguapo huobwa tsh 5000/ ya asante  na manesi na pindi akosapo hiyo hela hutolewa maneno machafu na matusi na kumkataza kumruhusu mpaka atoe hiyo hela./

 Mjadala huo  ulilenga   kuwahusisha wananchi na wahudumu wa idara ya afya kuweza kuachana na rushwa na kutoa huduma kwa jamii  ili kupata  taifa  endelevu na kufikia malengo ya mkukuta na malengo ya mileniamu.

Comments

  1. KWA UPANDE WANGU NINGEPENDA VIONGOZI WAWE MAKINI NA KAULI WANAZO ZITOA MAANA AKIFIKA SIKU AKASHIDWA KUWAJIBIKA TUNAHITAJI AWAJIBIKE,LAKINI EWE MKUUU NI KWELI TNZANIA HII HATUANA TABIA YA KKUJIWAJIBISHA CHUKUA HATUA UWE WA KWANZA WEWE.

    ReplyDelete
  2. UKWELI NI KWAMBA HIYO NI MANENO TUU MBONA VIONGOZI WA JUU WAMEFANYA MAMBO MENGI NA MAKUU YA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA LAKINI WAMESHIDWA KUWAJIBIKA SEBUSE WEWE ANZA TUTAKUONA.

    ReplyDelete
  3. KWA KWELI TUZINGATIE UONGOZI NA UTAWALA BORA HAYO MABILIONI MNAYOYACHEZEA MNAYATOA WAPI? NA KWANINI UNAWEKA KWENYE AKAUNTI ZA NJE NA SIO MUWEKE AKAUNTI ZA HAPA TANZANIA

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.