WANANCHI WA MLEMBULE WATEMBEA UMBALI WA KILOMETA 40 KUTAFUTA HUDUMA ZA AFYA.

www.facebook.com

WANANCHI wa kijiji cha  kijiji cha Mlembule  wilaya  ya Mpwapwa  Mkoa wa Dodoma Huwalazimu  kutembea umbali wa kilometa 12 hadi 40 kufika makao makuu wa wilaya kutafuta huduma za afya kutokana na kijiji  hicho kuto kuwa na kituo cha afya  katika kata hiyo kinachoweza kutoa huduma ya uapasuaji wa dharura kwa akina mama wajawazito.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji hicho  bwana Andason Mwangalimi  alisema  hali  hiyo imekuwa ikiwaathili sana  akina mama  wajawazito   wanapougua  usiku  au ugonjwa wa ghafla.
“Kutokana  na hali hii  akina mama huwalazimu kutembea umbali wa kilomita 12 hadi 40   kwasabu kijiji hiki  hakina zahati  na kipindi cha mvua kijiji hiki kinakorongo kubwa lijulikalo kama korongo la manamba  maji yakijaa watu hushidwa kuvuka na kuna mama mjamzito aliwahi kufia hapa  kutokana  na kukosa huduma kwa muda muafak”aliongea  .
Bwana Mwangalimi alisema kutokana  na hali  hiyo akina  Mama  wajawazito wamekuwa wakijifungulia njiani  na porini  kutokana na kuwepo  wa vituo vya afya.
Mmoja wa wananchi wa kata Bi Eva Deo alisema katika kipindi  cha masika wananchi wa kijiji hicho wanalazimika kutumia  dawa za mizizi ili kuweza kuokoa maisha yao kipindi cha masika .
Pia alisema kutokana kata hiyo huwalazimu watoto kuwapima uzito kwa kufunga mzani kwenye miti.
Mhuduma wa afya katika  kata hiyo Bi Halima Maganga alikiri kutoa huduma ya fya kwenye mti wa mkwaju aliopo kwenye  karibu  ofisi ya kijiji na alisema kwa mwezi mmoja anapima watoto 1400 hadi 1600.
Pia alisema akina mama wajawazito   kukosa faragha ya kupimwa kutokana na kupimwa kwenye chumba kidogo kisicho kuwa usiri na hadi ya kuwapimia akina mama wajawazito.
Bi Maganga alisema hata kama kuna mjamzito anahitaji msaada wa haraka   hushidwa kupatiwa msaada huo na kusababisha akina mama wengi wa kijiji hicho  kujifungulia kwa wakunga wa jadi na  majumbani kutokana na umbali wa huduma za afya zinako patikana.
Pia alisema akina mama wengi wamekuwa wakipata ugonjwa wa fistula  kutokana na wengi  kukaa na uchungu mda mrefu pindi wanapo safari,kukosa huduma za afya , na sehemu rafiki za kujifungulia.
Diwani  wa kata hiyo bwana Willison Mgunga  alisema kata hiyo  tayari  imesha  jenga  msingi wa jengo la zahanati na  wameshafyatua matofali 2748 ya sementi tayari kuanza kupandisha ukuta wa zahati ya kijiji hicho.
 Hata hivyo Mgunga alisema katika baeti ya halmasahauri ya mwaka 2017/2018 wametinga kiasi cha shilingi million 42 kwa ajili ya kuborsha huduma za afya katika kata yake.



Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.