WANANCHI WA WIYENZELE WAPATA HUDUMA ZA MAJI .


Zaidi ya wakazi  3,164  wa kijiji cha Wiyenzele kata  ya Chipogolo
wilaya  ya mpwapwa mkoni   Dodoma   wataondokana  adha ya kutafuta
maji umbali mrefu  uliokuwa unaikabili kata hiyo kwa muda mrefu baada
ya mradi  wa maji  ulio kuwa unajegwa  katika kijiji hicho  kukamilika
  na kuanza kutoa  huduma ya maji  kwa wananchi  kijiji hicho.
Mwandisi wa maji wilayni  hapa Bi Christina Mjengi  alisema kuwa kabla
ya mradi huo hali ya upatikanaji wa maji katika kijiji hicho ilikuwa
mbaya ambapo wananchi ilikuwa inawalazima kutumia maji ambayo sisafi
na salama  na wengine ilikuwa inawalazimu kutembea umbali mrefu
kutafuta huduma za  maji.
Alisema kuwa kukamilika kwa mradi utaongeza ukuaji wa uchumi wa kijiji
hicho kwa watu wa matumizi ya nyumbani pamoja na unyweshaji wa mifugo
.
Aidha alisema Mradi huo umetekelezwa kwa ufadhili wa program za maji
uliogharimu jumla ya shilling milioni 341,866,135/= (million mia tatu,
arobaini na moja laki nane sitini na sita elfu na mia moja therathini
na tano.
 Mwandisi mjengi alisema  mradi huo utawanifaisha wakazi wa kata hiyo
wapatao 3164 sawa na asilimia 93% ya wakazi wote  wa kijiji hicho na
unauwezo wa kuzalisha lita 90.000 kwa siku.
Aidha Mwandisi Mjengi alisema hadi sasa wilaya ya Mpwapwa imeweza
kufikia asilimia 51% za utoaji maji,ambapo alisema  vijijini ni
asilimia 32% mijini ni asilimia 70%.
Aliwataka wananchi wa  sehemu zenye miradi ya maji kuweza kutunza
mazingira  na vyanzo vya maji ili kuto kuhatarisha miradi  kukauka
kutokana na kukauka vyanzo vya maji  unaotokana na  uharibifu wa
mazingira.
Aidha alisema kuwa wameunda   vyombo huru vya watumiaji maji COWSO, na
kusema kuwa  kamti hizo zimeanza  kazi  ili kuweza kupunguza migogoro
kati ya vyombo vya watumiaji na kamati za maji.
Ameongeza kuwa katika mradi huo kulikuwa na shughuli kadhaa za kufanya
ambazo zilikuwa ni  kujenga tanki la kuhifadhia  maji lenye ujazo lita
90,000.ujenzi wa nyumba  ya kuhifadhia mashine  na kujenga  vituo  vya
kuchotea maji, na kusambaza mtandao wa mabomba   amabazo alisema zote
zimekamilika.
 Mmoja wa mwanakijiji Bi Anna Chisaluni   alisema kabla ya mradi huo
kukamilika   wakazi wa kijiji hicho  walikuwa wanatembea umabli wa km
tatu hadi tano kwenda kuchota maji katika  mabwawa ya kienyeji ambayo
maji hayo hayakuwa safi na salama kwa maisha ya  watu.
“ Visima hivyo ni vya kienyeji  Ng’ombe  ngedele  mafisi ya polini
walikuwa wanakunywa hapo na kujisadia humo ndio maji waliokuwa
wanayatumia  watu wa kijijini kwetu  na kupelekea kuwepo kwa magonjwa
mengi ya milipuko kama kichocho na  magonjwa ya tumbo”.aliongeza Bi
Chisaluni.
Pia  alidai  kijiji hicho kilikuwa kinakabiliwa na magojwa ya kuhara
ya mala kwa mala kitu walichokihisi kuwa kinasabishwa wakazi wa kijiji
hicho kutumia maji amabayo si  salama kwa matumizi ya binadamu.

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.