CHUO CHA MAZINGIRA CHAKABILIWA NA UCHAKAVU W MAJENGO.


CHUO cha  Sayansi ya   Afya  ya Mazingira  kilichopo wilayani Mpwapwa
mkoani Dodoma kinakadiliwa na uchakavu mkubwa wa  miundo mbinu ya chuo
hicho na kutishia afya  wanachuo chuoni hapo.
 Akitoa taarifa mbele ya mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir
Shekimweri mkuu wa chuo hicho  bwana  Rogasian Tarimo  alisema  chuo
hicho ambacho ni tawi la chuo kikuu cha  Muhimbili(MUHAS) kinachotoa
elimu ya AStashahada ya Aya ya mazingira.
Bwana Tarimo alisema  chuo hicho chenye wanachuo  54 kinakabiliwa na
uchakavu mkubwa wa miundo mbinu  na kutishia afya za wanachuo chuoni
hapo .
Aidha Tarimo alisema  chuo hicho tangu kifanyiwe ukarabati mdogo mwaka
2002  hakijafanyiwa  ukarabati tena na kupelekea miundo mbinu mingi
kuchakaa  na kushidwa kufanya kazi kiufanisi  kutokana na kuchaa sana
.
Alisema “sisi ni maafisa wa afya ya mazingira  ninaowafundisha ni
wataalamu wa afya ya mazingira sasa uchakavu huu hauendani na maudhui
ya chuo kwa maana miundo mbinu ya vyoo imechaa,vyumba vya madarasa  na
mabweni  hivyo kuniwia ngumu sana utekelezaji wa majukumu ya kila
siku”aliongea
Hata hivyo tarimo alisema pia chuo hicho kuto kuwa na hati ya umiliki
wa ardhi  kunachangamoto ya uvamivi wa maeneo ya chuo  na kutishia
kutokea kwa migogoro kati  ya chuo  na  watu na tasisi zilizo vamia
maeneo ya chuo.
Kwa  upande wake  mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana  Jabir Shekimweri
alisema  pamoja na chuo hicho kukabiliwa na  chanagamoto Lukuki
zikiwamo za watumishi  ameutaka uongozi wa chuo hicho kuongeza  nguvu
ya kukitangaza chuo hicho ili kuweza kuwa na watalaamu wengi katika
sayansi ya mazingira ambao kwa sasa taifa na dunia wanahitajika sana,
Pia Shakimweri alisema kuwa  kwa kushirikiana na uongozi wa chuo hicho
watajitahidi kushughulikia baadhi ya chanagamoto zikiwemo za watumishi
 kama dreva halmasahauri kuwaazima dreva wa chuo hicho ili kuweza
kuokoa gari  ya chuo hicho kuendelea kuchakaa bila kutumika kwa kigezo
cha kuto kuwa na dreva wa kuliendesha gari hilo.

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.