WAIMBAJI WA NYIMBO ZA DINI WAASWA KUFUATA MAADILI.



.
WAIMBAJI wa nyimbo za dini Nchini wamekumbushwa kutunga nyimbo za kuhamasisha Amani  na watu kupenda kufanya kazi.
Sambamba na hilo  pia waimbaji  wa kike wa  Music wa dini  wametakiwa  wasimame katika uwakili wa kazi ya  Mungu   ya kuomba kwa ajili ya Taifa  na kuombea familia na kubaki katika maadili ya music wao unavyo wataka .
Rai hiyo imetolewa jana wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma  na Meneja wa Bank  ya NMB  tawi la Mpwapwa Bi Beatrice Mwasa  katika Uzinduzi  wa  Album ya  mwimbaji wa nyimbo za Dini  Mwalimu  Paulina Ndatila(Mwl Boma) albam inayojulikana kwa jina la TUTATAWALA.
Bi Mwasa alisema kumekuwako  na upotovu wa maadili  kwa baadhi ya waimbaji wa nyimbo za dini kwa uvaaji wao ambao hauakisi kile wanacho kiimba
Pia alisema waimbaji hao wakitunga nyimbo za njisi ya kupunguza  migogoro  ya familia ambayo inatishia kuongezeka kwa  uvunjifu wa amani  kuanzia ngazi ya familia  hadi taifa .
Aidha Bi Mwassa alisema kama akina mama wakisimama katika kazi uwakili wao  wa kuzilea familia ,kukaa na watoto wao, na kuongea nao  kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza vitendo vinavyo tokea katika faifa kwa sasa  katika familia na ndani ya makanisa .
Bi Mwasa alisema  musiki wa nyimbo za Dini  kwa sasa ni miongoni mwa music unasikiizwa na  watu wengi  hapa nchini  hivyo  waimbaji watumie  fursa hiyo  kuhamasisha  Amani  na uwajibikaji kwa kufanya kazi “maana hata maandiko yanasema  asiyefanya kazi na asile,pia maandiko yanasema kuweni na amani  na watu  wote” aliongea .
Kwa upande wake   Kaimu Meneja wa  Benki ya Posta  mkoani Dodoma bwana Halfan Twaha alisema   Music ni fani  inayochukua kundi kubwa la vijana  na na watu wazima “ hivyo kuna haja ya serikali kuiwekea mazingira rafiki fani hii ili iweze kuzalisha  ajira kwa vijana wengi wenye vipaji vya uimbaji hapa nchini” aliongea
Pia alisema  kwa sasa Banki ya posta ambayo iko kwenye malekebisho makubwa inajipanga kufanya kazi na makundi yote wakiwamo wanamusic,wakulima ,wafanya biashara  pmoja na makundi yote ya watu wanaotaka kujiwekea akiba katika benk Posta Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.