DC MPWAPWA AOBWA KUINGILIA KATI MGOGORO WA ARDHI NDUGA.



   
WANANCHI wa kijiji cha Nduga kata Mlembule  wilaya ya  Mpwapwa Mkoani Dodoma  wameiomba kamati ya ulinzi na usalama kuingilia kati mgogoro wa mashamba katika bonde la  kijiji hicho unatishia uvunjifu wa amani.
Akiongea mmoja wa wananchi wa kijiji hicho na mwenyekiti CCM wa kijiji hicho Tumain Yohana amesema kumewako  hali ya sinto fahamu kutoka  mtu mmoja aliya fahamika kwa jina la Rashid Sudi Makasi    kwa wanachi  kile alicho kisema kuwa kunatishia  wananchi hao kuwafukuza kwa kuwafukuza katika maeneo yao kwa kudai kuwa ni yake.
Bwana Tumaini  amesema alisema kuwa kijiji cha nduga kimeanza kulitumia shamba hilo zaidi ya mika arobaini  iliyo pita na ilikuwa moja wapo ya chanzo cha mapato ya kijiji hicho ambapo wanannchi walikuwa wanakodishwa na kulipa kiasi kidogo kwa kijiji na sasa shmba hilo  linataka  kunyanganywa na bwana sudi kwa lengo  la yeye kutaka kuwakodisha wanakijiji hao.

 Mwanakijiji mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Hashimu Idd Risasi aMEdai kuwa  kijiji hicho kimaenza kumiliki eneo hilo kabla ya Tanganyika haijapata uhuru mwaka 1959 lakini mwaka 2014  alijitokeza mjanja mmoja ambae anawanunua viongozi wa kijiji na kutaka kupora eneo la serikali ya kijiji ambayo ni shamba la ujamaa tangia nchi hii inaitwa Tanganyika”aliongea
Bwana Risasi amesema kuwa  kwa sasa wameiomba serikali ichukuehatua za haraka kabla ya hali haijawa mbaya.
.Kwa upande wake  Diwani wa kata hiyo bwana Willson Mgunga amekili kuwepo kwa mgogoro ambao alisema kwa sasa unatishia amani ya kijiji hicho na  bwana Sudi.
Bwana Mgunga ameiomba serikali  kuchunguza nyaraka alizo kuwa nazo bwana Sudi juu ya umilikiwa eneo hilo  kwa kile kinachoaminiwa kuwa ni hati feki. Na kulipatia ufumbuzi wa haraka ili lisije kuleta madhara.
Alipo ulizwa juu ya tuhuma zinamkabiri bwana Rashid Sudi  Makasi amekanusha kuwanyanganya wananchi mashamba yao bali alisema maeneo hayo ni yake ya urithi wa baba yake na alisema “kwa yeyote anae dai kuwa eneo hilo ni lake aende mahakamani ndiko watakakoenda kutoa haki”.aliongea Bwana Sudi.

 …………………………………  MWISHOOOOOOO………………………








Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.