VIJANA WACHANGAMKIA NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA.




Idadi kubwa ya vijana wajitokeza kuchukua fomu  za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi  wa ndani ya  Chama cha mapindinduzi (CCM)  Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Katibu wa chama hichoi wilayani  Mpwapwa mkoani Dodoma Bi.Rukia  Hassan amedhitisha hilo kuwa idadi kubwa wa watu waliochukua fomu za kugombea  nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama ni kubwa ni   vijana .  
Bi Rukia amesema kuwa mchakato wa uchaguzi ulioanza  mwezi April mwaka huu katika ngazi za mashina  na kudhibitisha kuwa fofauti na miaka  iliyopita ambapo wanachma wengi wamejitokeza kugombea nafasi zauongozi ndani ya chama kwa kile alicho kisema kuwa ni kiashiria  cha Imani ya wanachama kurudi kwa chama.
Aidha amesema pamoja na kukua kwa imani ndani ya chama pia ni kuongezeka kwa uelewa Demokrasia  ndani ya chama pia kupunguza vikwazo vilivyo kuwa  vinakuwa  kipingamizi  kikubwa cha wanachamakuingia katika nyadhifa mbalimbali  ikiwemo Rushwa,Kujuana  na Upendeleo.
Pia Bi Rukia  amesema  kuwa Imani ilionyeshwa na mwenyekiti wa chama Taifa ambaeni Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuri  imeweza kurudisha Imani ya vijana kurudi ndani ya chama  na kugombea nafasi ndani ya chama.
Hata hivyo Bi Rukia amewahadaharisha  wagombea wote watakao kiuka  taratibu na kanuni cha uchaguzi kuondolewa katika kinyang’anyilo hicho.
Pamoja na idadi kubwa ya wanachama hao kujitokeza kuchukua fomu kwa wingi chombo hiki kimebaini kuwapo kwa  changamoto ya    kubaguana kijimbo kitu kinacho ashirilia kumeguka kwa chama.

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.