WANANCHI WA IGOVU WAMTUMBUA MWENYEKITI WAO.




WANANCHI wa kijiji Igovu  wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma wamemtaka mwenyekiti wa mtaa bwana Yunis Mwagowa  achie ngazi kwa kujiuzuru  kupisha uchunguzi kutokana na kutuhumiwa kutumia fedha za mapato ya kijiji shilingi million moja laki tano na elfu hamsini (1,550,000)na kutoitisha mikutano ya  kisheria ya kusoma mapato na matumizi.
Mbali ya kumtaka mwenyekiti huyo aachie ngazi pia wamemtaka  aurudishe pesa zote kiasi cha shilingi million 1550,000/= zilizotegwa  kwa ajili ya kuboresha huduma za kimaendeleo katika  mtaa huo.
Hatua hiyo walifikia kwenye mkutano wa hadahara mala baada ya mwenye kiti huo kusoma tarifa mapato na matumizi  ya mtaa huo ambapo taarifa yake ilizua maswali mengi yaliyo kosa majibu  na  kupelekea wananchi hao kuikataa taarifa hiyo na kuwataka  wakaguzi wa ndani wa halmasahauri kufanya ukaguzi maluum wa mapato na matumizi ya mtaa huo.
Akongea mmoja wa wananchi wa kijiji hicho  Paskal Mbeho aMEsema  mwenyekiti wa mtaa huo amekuwa haitishi vikao vya kisheria vya  kila baada ya miezi mitatu lakini vilikuwa havifanyiki  na kusababisha mwenyekiti wa mtaa huo kufanya maamuzi peke yake bila kushirikisha uongozi wa mtaa.
 Pia amesema katika taarifa yake inaonyesha amenunua vitu vya kusaidia kijiji ambayo havilingani na fedha  iliyotumika  na vitu vinavyo onekana katika uharisia.
Wananchi wa kiji hicho wameenda mbali zaidi na kiutaka tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wilayani hapa  kuweza kuichunguza  zaidi manunuzi hayo yaliyo fanywa na mwenyekiti huyo kwa kile walicho kisema amenunua risiti za malipo ili kuoanisha fedha iliyo andikwa kwenye risiti na vitu halisi.
Aidha  Mbeho amesema wapo viongozi kwa kutumia  madaraka waliyopewa na wananchi wamekuwa wakijinufaisha na baadhi mapato ya mtaa huo huku wananchi walegwa wakishidwa kupata   huduma muhimu,
“Hayo ni matumizi mabaya ya madaraka kwa viongozi ambao  wamepewa madaraka na wananchi  lakini wamegeuka kuwa mamwinyi  na kuanza kuhujumu wananchi hivyo tunaiomba TAKUKURU ijaribu kulichunguza suala hili”Mbeho
 Kwa upande wake mtendaji wa kijiji hicho  Bi Nola Rorbart amekili kuwepo kwa changamoto hiyo  kutoka kwa wanakijiji  ambayo wanamtaka mwenyekiti wao aitishe mkutano wa hadhara wa kusoma mapato na matumizi ya mtaa huo lakini bila mafanikio.
“Ukweli ni kwamba  wenye viti wa mitaa yote mitatu igovu ,Ng,ambo,na National Housing bila kutisha ilibidi mimi niitishe mikutano ya mitaa yote ya mitaa mitatu ya kusoma mapato na matumizi lakini wananchi wameikataa taarifa ya Igovu na sio mitaa minginezilikubaliwa”aliongea  bi Norah

Pia   amekili   wananchi hao kumsimamisha kwa muda  mwenyekiti wa mtaa wa Igovu wa kwa kupisha uchunguzi  hadi hapo taarifa itakapo  tolewa na alisema tayari mwenyekiti huyo amesharudisha mihuri ofisini kwa mtendaji wa kata.
 Pia lisema  kuwa     suuala hilo limefika  kwa uongozi wa juu wa halmasahauri na lakini wanasubiri maamuzi ya wananchi hao.
Ukweli  wenyeviti wote watatu wameandikiwa barua na mtendaji wa kata  ya kuwataka wapeleke mapato na matumizi  yote ya kijiji kwa muda wa mwaka mmoja na kuitisha mikutano  ya hadahara ya kuwasomea wananchi mapato na matumizi mala muda unapofika.
Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa huo bwana Yunis  Mwagowa    lakini amekanusha kutumia pesa hiyo ya kijiji kwa maslahi yake binafsi bali alisema ni wananchi kuto kuhudhuria  katika mikutano ya hadhara  ambayo inakuwa inasoma mapato na matumizi.
Pia aliongeza kuwa  suula hilo linapewa nguvu na baadhi wa wapinzani wake ili kumtaka aondoke madarakani kwa hila kitu alichokisema kuwa  ni siasa chafu ambazo zinaendeshwa juu yake.
Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.