SERIKALI ISHUGHULIKIE VYANZO VYA MADAWA YA KULEVYA SIO MATOKEO.

Na Stephen noel- mpwapwa.
SERIKALI imeswa kuachakuwekezanguvu kubwa katika kushughulikia matokea ya madawa ya kulevya nchini bali ijikite  na kuongeza nguvu katika kushughulikia vyanzo vya madawa ya kulevya ili kuweza kuliokoa Taifa.
Wito huo umetolewa na bwana  Elieza Mdakilwa  mwenyekiti wa  shirika la (TUSPO)Tanzania usersand survivors psychiatry ambalo ni shirika lisilokuwa la kiserikali  la kuwahudumia watu wenye matatizo ya akili  na kupambana na madawa ya kulevya   kwenye semina  ya siku mojailiyo fanyika katika hotel Akh  juu ya kuwasaidia watu wenye magojwa ya akili.
Mdakilwa amesema kuwa  pamoja na serikali kuonyesha jitihada kubwa katika kupambana na wimbi la madwa ya kulevya nchini bali amesema kuwa jitihada hizo zinaonyesha kujikita kupambana na matokeo yake badala kushughulikia  vyanzo vikubwa vya tatizo hilo.
Mmoja wa wa wajumbe katika semina hiyo Bi Teresia  Mnemele amesema kuwa  kumekuwako na  wimbi kubwa  watu wenye  ugonjwa wa akili kwa sasa ambao  matatizo hayo yamezi kukua siku hadi kutokana na  ongezeko kubwa la vijana kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya   ikiwamo  madawa ya viwandani na madawa ya masahamabani .
Pia alisema “kwa sasa jamani  vijana wa kike kwa wa kiume wameharibiwa na madawa ya kulevya  na kwakweli madwahaya yanathiri sana nguvu kazi ya taiafa  kwa asilimia nyingi lakini sisi kama wananchi vyombo hivy vya kushughulikia sula hili wako wapi mbona tunasikia wamekamata kete kumi,wale wanaokamatwa na kilo 100,mbona hatuwaoni wakipelekwa mahakamani”alihoji  bi Teresia.
Kwa  upande wake Mratibu wa  wa shirika hilo tawi la Mpwapwa bwana Amos  Nyongole  alisema kuwa kwa mujibu wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu    inawataka nchi wanachama ikiwamo  Tanzania inawataka nchi wanachama kuweza kufuata na kuzinagatia  mkataba huo ili watu waliokuwa kwenye kundi hilo  kuweza kupata haki zao.
Aidha   Nyongole alisema mradi  huo ulifadhiliwa na shirika la Foundation for civil society imekusudia  kuamsha uelewa  wa sheria ya mpya ya afya ya akili  no 21 iliyopitishwa na  na bunge  mwaka 2008 ikiwa na lengo la kuhakikisha  wagonjwa wa akili  nchini  wanaboreshewa  haki  na mahitaji  yao .
Hata hivyo  ofisa ustawi wa jamii  wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Anton Mbambile  alisema kuwa  lazima jamii iunganishe nguvu kupambana na madawa ya kelevya lakini pia kuto kuwaficha na kuwanyanyapaa watu wenye matatizo ya afya ya akili.

Pia Mbabile  amesema lazima jamii kuweza kuunganisha nguvu kuwafichua wauzaji wa madawa ya kulevya na wazalishaji  ili kuweza kupunguza tatitizo hilo ambalo linatishia uendelevu wa rasilimali watu kwa siku za mbeleni.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.