WALIMU WAASWA MAADILI



 Na Stephen Noel – Mpwapwa.
WALIMU watakao husikana kusimamia    mitihani ya  kidato cha nne mwaka 2016  wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma  wametakiwa  kufanya kazi hiyo  kwa kuzingatia maadili  na maelekezo  wa kati  wote yanayo tolewa  ili kufanikisha kazi  hiyo kufanyikabila  ya kuwapo kwa kasoro zozote.
Akifungua  Semina  ya wasimamizi wa mtihani wa kidato cha nne  kwa mwaka 2016  iliyo fanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Mpwapwa mkuu wa wilaya ya Mpwapwa  Jabil Shekimweri  amesema Serikali ina imani kubwa na walimu hao kufanikisha zoezi hilo la kitaifa  pia na wao hawana budu kuonyesha imani hiyo  kwa kutekeleza majikumu yatakayopewa  na viongozi wao pamoja na kamati ya mtihani ya mkoa na wilaya.
Amesema dhumuni la semina hiyo ni kuwakumbusha  na kuwalekeza wazimamizi wote wa mitihani  pamoja na wakuu wa shule kuto kufanya udanganyifu wowote wawapo katika vituo vyao vya mitihani ili kulisaidia taifa kuweza kupata  wanafunzi halali na sahihi ambao watakao kuwa wataalamu wa baadae katika serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Amewataka  wakuu wa shule wote kwa kusaidiana na waratibu elimu kata kuweza kuwachukulia hatua wazazi na walezi wote ambao tayari wamewaowesha wanafunzi  na kusabisha wanafunzi hao kuacha shule.
Kwa upande wake Ofisa elimu sekondari wilayani hapa Bi Suma  Mwapulo  alisema kuwa wa mwaka 2016  jumla ya watahiniwa  1663 wanategemea kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa kujitemea .
Bi Mwapulo amesema wanafunzi  61 wanatarajiwa kufanya mtihani wa maarifa katika kituo cha kufanyia mitihani katika chuo cha ualimu mpwapwa na wanafunzi  84 ni wanafunzi  kidato cha nne ambao watafanya mtihani kama wanafunzi wa kujitemea wakatika wanafunzi 1579 ni watahiniwa wa shule za sekonadri za serikali na za  Umma .

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.