WAKAZI WA MAJENGO MPWAPWA WATHILIWA NA MOSHO WA TAKA




WANANCHI wa mtaa wa majengo katika kata ya Mpwapwa mjini  wilayani hapa wamelalamikia kitendo cha  uongozi wa wilaya kuweka dampo la kuteketezea taka  katika maeneneo ya makazi ya watu.
Kedmoni Mapuga  mkazi wa  mtaa huo alisema kumewako  na  usumbufu mkubwa  na badhii ya wakazi wa mtaa huo wenye watoto wadogo huwalazimu kuhama nyumba  kutokan na moshi huo kuathiri kiafya  na kusababisha vikozi kwa watu wazima na watoto.
Mapuga alisema  baada  kuwa  wakazi wa mtaa wa majengo  wamekuwa wakiadhiriwa na moshi mkali na wenye harufu kali na kutishia wakazi wa  mtaa huo kupata ugonjwa wa kifua kikuu   kama bado halimasahauri ikiendelea kuchoma taka katika eneo la korongo ambalo liko katikati ya  makazi ya watu .
Aidha Mapuga  ameenda mbali na kuulalamikia uongozi wa  halmasahauri kitengo cha usafi na mazingira kwa kusema kuwa wameshidwa kutekeleza na kuendana na kauli ya  raisi Magufuli ya  kuwataka wanachi kufanya usafi  ili kuweza kuweza  kujikinga na magonjwa yanayoweza kusabaishwa na uchafu.
Pia aliema  uchafu huo unatupwa katika  eneo hilo linatishia  kuweza kutokea magonjwa ya mlipuko katika kipindi hiki cha kuelekea  msimu wa mvua za masika.
Kwa upande wake mwenyekiti wa  mtaa huo Bi Asha Makupa  amekili mtaa wake kuadhiliwa na kadhia hiyo kitu alicho kisema kuwa takataka nyingi zinazochomewa katika eneo hilo zinazalishwa  na wafanya  biashara wa sokoni  na kuzitupa katika korongo hilo.
Bi Makupa amesema alisema suala hilo amelifikisha katika uongozi wa halamasahauri lakini  alijibiwa kuwa chanagamoto ni halmasahauri kuto kuwa na gari la kusombelea taka na kwenda kuzitupa kwenye eneo la dampo lililoko nje kidogo ya mji wa Mpwapwa.
Naye katibu wa soko kuu la Mpwapwa mjini bwana Said Sadala alikili baadhi ya taka laini kuzitupa  katika eneo hilo kitu alicho kisema kuwa ni kutoakna na  kuruhusiwa na uongozi wa mamlaka wa mji  kutokanana  kukosekana kwa miundo mbinu ya kubebea bithaa hiyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa  mji  mdogo wa Mpwapwa bwana Hamis Hoper amekili kuchomea takataka katika  maeneo ya watu kitu alicho kisema kuwa kinatokana na uongozi wa mji huo na uongozi wa halmasahauri ya wilaya kutokuwa na magari ya kusombea taka  na kwenda kuzitupa dampo.


Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.