KILIMO CHA UMWAGILIAJI NDIO WAROBAIN WA USALA WA CHAKULA TANZANIA




Na stephen noel  Mpwapwa .
SERIKALI ya awamu ya tano  imeaswa kuwekeza katika  tafiti   za  kilimo na mifugo hapa nchini ili kuweza kuwa na uhakika na usalama wa chakula kwa wanachi wake.
Kauli hiyo ilitolewa jana na  mkurugenzi mtendaji wa  utafiti  Tanzania  Dr,Daniel Komuhangilo alipokuwa akifungua  warsha ya siku tatu ya   kwa watafiti  juu ya  maabara za kielektroniki   iliyo fanyika katika ukumbi wa mikutano katika chuo cha utafoti cha  TALIRI Mpwapwa.
Dtk.Komuhangilo   alisema  kwa mujibu wa tafiti zilifanywa hapa nchini zinaonyesha  kuwa mabadiliko ya   tabia ya nchi  ni miongoni mwa sababu kubwa  zinazopelekea Tanzania kushidwa kuwa na uhakika wa chakula .
Aidha Dkt. Komuhangilo  alisema   kuwa  Tanzania  ni miongoni wa  nchi ambyo  idadi kubwa ya wanachi wake wamejikita katika sekta ya kilimo na mifugo  ambayo inakadiliwa zaidi ya  asilimia 80% ya watanzania wanajishughulisha  na sekta ya kilimo na mifugo   japo kuwa bado sekta hii haijaonyesha  mafanikio makubwa sana  kwa wanachi wake.
Mwezeshaji  kwenye warsha  Prf. Frankwell  Dule  kutoka  chuo kikuu  cha kilimo cha  Sokoine  alisema  ili kuweza kuwa na kilimo chenye tija lazima  serikali iwekeze kwenye kilimo cha umwagiliaji  ambacho pekee ndicho kitakuwa suruhisho la kuwa na usalama na uhakika wa chakula  katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabia ya nchi.
Prf. Dule  alisema kuwa changamoto ya uwajibikaji wa maafisa ughani  ngazi ya jamii inapelekea  sekta ya kilimo  kuonekana  kuto kuonyesha  tija katika miaka yote ya uhuru wa nchi  japo kuwa na kauli mbiu lukkuki za kuhamisisha sekta ya kilimo  bila kuwapo na mikakati ya kuboresha sekta hiyo.
Hata hivyo hivyo Prf.Dule  alisema chanaga moto ya  mbegu feki, viwatilifu feki, na wakulima  kushidwa kubadilika  na kuendelea kulima kimazoea  na kufuga kimazoea pia ni sababu zinazo pelekea kilimo  kushidwa  kusonga mbele kwa  miaka  zaidi ya hamasini sasa.
Kwa upande wake mratibu wa warsha hiyo na  ofisa maabara za kielektonik  katika tasisi ya  TALIRI Mpwapwa Bi Neema Urasa  alisema kuwa warsha hiyo imelenga kuwajengea uwezo watafiti  kubadilishana uzoezu kwa njia za kielektrik kwa  kusambaza taariza za kitafiti  katika machapisho ya tafiti za kisayansi
Pia alisema njia hiyo inawasaidia watafiti kutumia rasilimali chache ikiwemo muda, fedha, na watu ili kuweza  kufikia malengo kusudiwa.
Hivyo alisema nchi zote zilizo wekeza katika  tafiti na kuzitumia tafiti za wataalmu katika maamuzi zimesonga mbele  kimaendeleo ya jamii,  Siasa Pamoja na kiuchumi.
s

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.