MTENDAJI WA KIJIJI AMUWEKA MAHABUSU MWANAFUNZI KWA SIKU TATU RUDI.




KATIKA hali isiyo kuwa ya kawaida  mtendaji wa jijiji  cha Igunga kata ya Rudi  wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma  amemuweka maabusu  kwa siku  tatu mtoto  ya  miaka 11  mwanafunzi wa darasa la tatu  mala baada ya kupigana  na mwezie shuleni.
Mzazi wa mtoto huyo bwana Gerard  Simbai  alisema  kuwa    watoto hao  wanaosoma katika shule ya msingi Igunga  kata Rudi  walipigina  wakiwa shuleni  siku ya tarehe 30,agosti mwaka huu lakini mtoto huyo alikamatwa siku  ya taehe 11,octeber  mwakaa huu.
Bwana Sambai alisema baada ya kukamatwa na mgambo aliyejulikana kwa kwa jina la moja la  Dales   na kumwambia   kuwa  mtoto huyo anatakiwa na  na mtendaji  wa kijiji  kwa mahojiano zaidi aliye julikana kwa jina la Makalios Mbada.
Aidha bwana Sambai alisema alipo jaribu kumfuatilia haki  ya   mwanae uongozi wa kijiji hicho ilimtishia  na kumtaka alipe gharama za matibabu alizotumia  mzazi wa mtoto walio pigana na mwanae  ili wamuachilie  alipo kataa  kulipa ghalama hizo ndipo alipo chukua jukumu la kumchukua mtoto na kwenda kumuweka chini ya ulinzi wa mgambo wa kike kwa siku tatu mfululizo.
Pia  Sambai  alisema kuwa tangu tukio hilo kutokea  lakini uongozi huo ulikuja kumkamata mtoto huyo  baada ya mwezi mmoja na zaidi kupita  na ndipo kumshikilia  na kumuweka chini ya ulinzi.
Bi  Mwaka anaetumika kama mgambo katika kijiji hicho japo hajapitia mafunzo ya mgambo  alikili kumshikilia mtoto huyo kwa siku tatu mfululizo mala baada ya kupigana na mwezie shuleni na kuumizana  kwa maelekezo ya  mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wa kijiji.
“Kwa kweli mimi niliambiwa nikae na mtoto huyo hadi hapa mtendaji atakapo kuja kumchukua nimekaa nae siku mbili nikaona kimya ilibidi niende kuwambia lakini mwenyekiti wa kijiji aliniambia nikimuachilia nitafugwa mimi ndipo nilipo enda kwa mtendaji wa kata aliye amuru mtoto huyo kuachiliwa na kuwakabithi wazazi wake” aliongea Bi Mwaka .
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igunga   mwalimu Egid Mwachali  alikili siku ya taerehe 30 septemba mwakaa huu watoto hao wakiwa shuleni  na mmoja alipiga mwezie kichwa   na wote waliitwa na kuonywa na walimu  lakini  suala hilo lilishia hapo
Aidha mwalimu Mwachali  alisema  kwama baada  muda kupita zaidi ya mwezi ndipo alipo ona mtoto huyo huyo hakufika shuleni kwa muda wa siku tatu na alipo fuatilia aliambiwa anashiliwana  na mtendaji wa kijiji kwa kile alicho kisema kuwa  ni kutokana na  ugomvi ilio tokana na kupigana na mwezie shuleni.
Aidha  Mwalimu Mwachali  alisema kuwa” kwa mujibu wa  sheria ya mtoto  ya mwaka 2009  inakazata kumuweka chuni ya ulinzi mtoto yeyote chini ya miaka 18  na kumachisha masomo bila  taarifa kwa kosa olote lile kitendo cha namana hiyo ni ukatili kwa watoto lakini pia ni kuwaathili watoto kisaikolojia”aliongea mwalimu mwachali
Kwa upande wake mtendaji wa kata ya Rudi  bwana Harod Mkombola  alikili mtoto huyo kushilikiliwa  na uongozi wa kijiji cha Igunga  kwa siku mbili na alisema kuwa yeye hakuwa na taarifa  baada ya kupata taarifa iliamuru mtoto huyo kuachiliwa  na kukabidhi kwa wazazi wake.
Alisema uongozi wa kijiji hicho uliamua kumshilia mtoto huyo baada ya kuona mtoto mwezie kulalamika kuumizwa kichwani na kuhitaji vipimo zaidi katika hospitali ya  rufaa Dodoma.


Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.