WAWEZESHESHAJI WA TASAF WATAKIWA KUSIMAMIA TARATIBU



WAWEZESHAJI  wa wilaya  katika mpango wa TASAF  awamu ya Tatu  wametakiwa  kusimamia  taratibu  na kanuni za mpango huo  ili uweze kuwanufaisha walegwa kama ilivyo kusudiwa na  serikali.
Kauli hiyo  ilitolewa na   afisa ufuatiliaji  wa mpango huo wilayani hapa Fraston Anyitike  alikuwa akingea  na wawezeshaji  wa wialaya katika mpango wa malipo  juu ya kuwezesha kaya maskini  katika kipindi cha roya ya  march  -April  2015.
Anyitike amesema japo kuwa utaratibu unafahamika  lakini wapo baadhi ya  watendaji wa vijiji wamekuwa wakitumia  fulsa hiyo  kuwaingizia wanachi  michango mbalimbali ambayo haipo katika  mpango  wa  vipaumbele vya  ruzuku hiyo kwa  walegwa.
Amesema kuwa ruzuku ya  wanayao pokea walegwa  katika  mpango wa TASAF  awamu ya tatu  imelenga kuboresha  elimu na afya kwa kaya hizo  na kuongeza kipato  kwa kaya  maskini  kupitia  uwekaji wa akiba na kuwekeza katika shughuli za kiuchumi kama ufugaji wa kuku wa kienyeji ,ufugaji wa nguruwe na mbuzi kwa kaya hizo ili  ziweze kuboresha  maisha.
Mmoja wa wanufaika wa   mpango katika kijiji cha iyenge Bi Maria Vitalo  amesema pamoja na Tasaf kuhamasisha  walegwa kukata bima  wamejitokeza  kukata bima hizo lakini tatizo  tangu wakatiwe bima hizo hawajapewa  vitanbulisho vya matibabu  na hivyo kuendelea kununua dawa katika  maduka ya dawa wakati  walikata  bima miezi mitatu iliyo pita.
Mtendaji wa kijiji hicho Enock Kinoga  amesema  kumekuwako na changamoto ya  ya ukosefu wa vifaa vya kutengenezea  vitambulisho hivyo na alikili kuwepo kwa usumbufu mkubwa kwa wanachama hao kushidwa kupata huduma katika vituo vya  afya  kutokana na kukosa  vitambuliso .
Kaimu mratibu wa mfuko wa afya ya jamii wilaya  Bwana Musa Pima amekili kuishishiwa  vifaa hivyo  ikiwemo  karatasi za  kugundishia zijulikanazo kama  lamination  kitu alicho kisema tayari wamesha pokea  karatasi hizo  na wamesha  anza kuzisamabaza  katika  vituo mablimbali hapa wilayani.



Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.