MADREVA WA BODABODA WAPIGWA MSASA MPWAPWA.



Na  Stephen noel mpwapwa.
MADEREVA wote wa naoendesha vyombo vya moto wametakiwa kuzingatia  sheria  na alama za barabarani  ili kuweza kupunguza ajali sisizo kuwa za lazima kwa lengo kuakoa maisha ya watu na mali zao.
Kauli hiyo imetolewa na  mkuu wa wa usalama  barabarani wilyani mpwapwa  Josephat Mjema alipokuwa akifungua mafunzo  ya siku saba ya  waendesha vitu  vya moto na wamiliki wa vitu vya moto na mafunzo yanayoendeshwa na shirika lisilo kuwa la kiserikali la  APEK.
Aidha  Mjema alisema  jeshi la polisi limeingia mkataba  na shirika lisilokuwa la kiserikali  la APEK   kutoa mafunzo ya  usalama barabarani  kwa madreva wote wa naoendesha vitu vya moto , wanajamii ,na wamiliki wa vitu vya moto  kwa lengo la kuweza kupunguza ajili  za barabarani.
Mjema alisema  kutokana na tafiti  zilizofanywa  na jeshi la polisi  wamegundua kuwa ajili nyingi zinazotokea  barabara  zinasababishwa na madreva kupuuzia  sheria za barabarani na alama za barabarani.
Pia alisema mbali  na sababu hizo  kuna sababu niyngine kama za ubovu wa miundo mbinu na ubovu ya vifaa vya moto  ambazo hutokea mala chache sana lakini alaisema ajali nyingi husababishwa na madreva  kwa kuto kuzingatia  sheria  na taratibu za barabarani.
Desdery Kyayonka  mkufunzi katika  semina  hiyo  alisema mada zitakavyo fundishwa ni sheria za usalama barabarani, alama za usalama barabarani, ujasilia mali, na dhana ya pilisi jamii kwa muda  wa siku saba.
 Kayonka alisema  kumekuwako na mwitikio mdogo wa  wa watu wanao endesha vitu vya moto  hasa wanaoendesha pikipiki za magurudumu mawili bodaboda  kuhudhuria mafunzo hayo  kitu alichowataka kuhudhuria mafunzo hayo ambayo alisema yanafaida kubwa sana kwao na kuwarahisishia upatikanaji wa leseni za udreva.
K wa upande wake askari wa usalama barabarani wilyani hapa  Novaty Magoma  alisema  watapisha msako mkali kwa madreva wote wasiokuwa na leseni na wanaendesha vitu vya moto  na hawajahudhuria mafunzo hayo .
Magoma alitumia fursa hiyo  kuwataka madreva wote wa  bodaboda kutii sheria bila shuruti na kupunguza  misaha ambayo inaghalimu maisha wa watu na mali zao  hivyo alimewataka madreva wote kuhudhuria mafunzo hayo.
Mmoja wa wanasemina hiyo Letisia Mwenda  alisema pamoja na kuwapo kwa  mafunzo hayo  yatawajengea uwezo wa kuelewa sheria ambazo  baadhi ya maaskari wamekuwa wakitumia  mmuanya wa  huo kuwanyanyasa  na kuwageuza baadhi ya waendesha bodaboda kama mitaji yao ya kujipatia kipato chao  cha kila siku.
Pia Letisia amewataka  madreva  wenzake kuweza  kuhudhuria  mafunzo hayo ambayo alisema kuwa yanamanufaa makubwa  kwa ajili ya maisha yao na mali zao na mali za matajili wao.


Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.