BILION MOJA ZATOLEWA KAMA MKOPO NA FINCA MPWAPWA



 Na Stephen noel –Mpwapwa.
JUMLA  ya shilingi  bilioni moja na   na million miatano zilitolewa kama mkopo mbalimbali na Benk Finca  tawi la Mpwapwa Mkoa wa Dodoma  kwa wateja  wake wapatao 2000 kwa mwaka 2013/2014.
Kauli hiyo ilibainishwa na meneja wa Finca tawi la Mpwapwa  Bw,Edson  Joel alipokuwa akiongea na waaandishi wa habari  ofisini kwake  jana  kwa mahojiano maluum.
Joel alisema mikopo walioyo itoa ni kwa ajili ya biashara kwa wafanya biashara   wakubwa wa kati, na wajasilia mali wadogo wa wilaya ya mpwapwa.
Meneja huyo alisema  Lengo la  Benk hiyo  ni  kukuza  biashara na  kuimarisha uchumi kwa jamii na pia  kuondoa umaskini  kwa watanzania  ambao  wengi wao hufanya kazi  ya kupambana na umaskini lakini hukabaliwa na chanagamoto ya ukosefu wa mikopo na   elimu ya ujasilia mali .
Amesema wao kama wadau  huwasaidia serikali katika kutekeleza malengo ya mileniam na kuweza nchi ya T anzania   kufikia kipato cha kati ifikapo 2025 ili kuweza kupunguza  umaskini  wa kaya na jamii  kwa  kuwasaidia wengi hasa akina mama  kuweza  kumiliki biashara zao.
Mmoja wa wa wajasilia  mali ambae hakutaka jina lake lifahamike alisema Tasisi nyingi za kifedha hazina lengo la kuisaidia wajasilia mali bali wamelenga  kujinufaisha zaidi na kupata faida  kubwa kutoka kwa wateja wao wanaowahudumia
Alidai kuwa Tanzania huenda ikashidwa kufikia malengo yake ya Milenium na Mkakati wa kuondoa na kupunguza umaskini tanzania  kutoaka na Tassisi nyingi za kifedha  kutoza riba kubwa  kwa wajasilia mali wadogo wanaokopa katika tasisi hizo.
Alisema lengo ambalo hupatiwa wasiwasi wa kuto kufikiwa ni lengo la kwanza la mileniamu linalo dai kuondoa umaskini wa kipatao na njaa na  kwa kutuza  riba kubwa zaidi ambayo ni digiti mbili kitu alicho iomba  serikali kuzitembelea tasisi hizo  na kujua mifumo ya  Tasisi hizo.
Aidha  Joel alisema kuwa  mbali  ya kuwa na  akina mama wengi wenye   uhitaji mkubwa wa kukuza uchumi wa familia  na  jamii lakini  wanakabili na na changamoto kubwa ya mfumo dume  unaoikandamiza jamii  hasa mwanamke kuruhusiwa kuingia katika tasisi za  kifedha  na waume zao kutokana na  uelewa mdogo wa wanaume juu ya benk ya finca .
Alisema  mikopo walio itoa kwa wakazi wa Mpwapwa umesaidia kubadilisha  maisha  ya wakazi hao kwa kukuza biashara zao  na  kuweza kufanya shughuli zingine za kmaendeleo kama kusomesha watoto na kujenga nyumba bora.
Pia  aliongeza  pamoja na  mafanikio hayo bali wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo watanzania wengi  kuto kuzitumia  tasisi za kibenki katika kutunza  fedha zao  kitu alichokisema kuwa  kinaongeza uhalifu katika jamii na mauwaji kutokana  watu wengi kutunza fedha majumbani.
Alisema  kuwa  kwa mujibu wa tafiti zilizo fanywa na  Benki ya kuu ya Tanzania  ni asilimia  14% tu ya watanzania ndio hutumia   tasisi za kibenk katika kutunza fedha zao.
Amedai kuwa  jamii iondoe dhana  ya kuwa  Finca hutoa riba kubwa kwa mikopo yao kitu alichokanusha kuwa benk  hiyo hutoa riba kidogo ambapo alisema kila  laki moja atakayo chukua mteja hulazimika  kulipa shilling 3000 kwa mwezi ambayo alisema sawa na shilingi elfu 18,000/= kwa miezi sita.
Meneja huyo amewataka wana Mpwapwa ambao ni jamii wa wafugaji kuweza  kuvuna kwa kupunguza mifugo yao  kuweka fedha benk ili kuweza kujipatia kamisheni za faida kwenye akaunti  ya malengo.

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.