TASAF YASAIDIA KAYA MASKINI 6288 MPWAPWA



Na Stephen noel – MPWAPWA
HALMASHAURI ya wilaya ya mpwapwa  mkoani Dodoma  imeanza kunufaisha kaya  maskini 6288zenye kipato  cha chini  kwa kuzipatia  fedha  za kujikimu  kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF  awamu ya nne.
Gazeti hili limejaribu kutembelea kaya  maskini katika vijiji mbalimbali  vilivyo kuwa chini ya mrad na kukutatana na walegwa  ambao walikiri mpango huo tangu uanze kutekelezwa umeweza kubadilisha maisha yao  na sasa kuyaona kuwa maisha yao yamekuwa na unafuu  tofuati na hapo awali.
Mmoja wa wanakijiji cha vighawe  kata ya vighawe Mery Mazanda amesema  awali  alikuwa ankula mlo mmoja kwa siku   lakini tangu mradi huo uanze kutekelezwa nay eye kuingia kwenye mpango kumeweza kubadilisha maisha yake na  afya yake imeboreka  kwa kuweza kula milo mitatu kwa siku.
Amedai ‘”kuwaa  sasa anaishukuru serikali ya  Tanzania  kwa maana  isingekuwa hivyo sisi wanyonge tungekuwa tumekufa maana nilikuwa nakula mlo mmoja wa siku tu na siku zingine  tangia asubu hi hadi asubuhi nyingine  bila kula kitu  kipindi cha ubuyu nilikuwa nashindia ubuyu ambao bila kula chakula unalevya, kwa kweli  sasa naishukuru mno serikali ya Kikwete”.
Mwezeshaji  wilaya Protasia  Makumbo amewataka  wanufaika hao kuweza kuanza kubuni miradi mbalimbali ya  kufuga kuku ngombe na nguruwe ili waweze kuwa  na miradi endelevu.
Pia diwani wa kata ya vighawe Dikson Mahuwi amesema kuwa mpango huo umewasidia wanufaika wengi ambao sasa wengi wao wameonyesha mabadiliko  makubwa kwa kujenga nyumba bora, kuibuia miradi midogomidogo ambayo wanaitumia ili kuweza kujikimu katika maisha yao ya kila siku.
Mratibu wa  Tasaf  wiliya ya Mpwapwa Bahati Magumula  alisema katika robo ya nne Watoa   ruzuku kwa kaya 6288  zitakazo nufaika na mradi huo kwa kaya maskini zilizo ibuliwa kwenye zoezi la uandikishwaji  wa zoezi hili hapa awali.
“Kwa awamu hii tunatoa ruzuku hii kama  shughuli za kawaida kwa robo hii ambapo tutatoa kiasi cha shilingi million 190.3 kwa kaya legwa 6288”alielieleza Magumula
Aidha  Magumula  alisema hapa awali kuna baadhi ya kaya zilikataa kuingia kwenye zoezi hili lakini baada ya kuona mafanikio kwa wenzao wameanza kusumbua na wao kutaka kuingia kwenye mpango  ambapo inachukua muda mrefu sana kurudishwa  kwenye mpango.
Kwa upande   afisa Ufuatiliaji wa Tasaf  wilayani hapa Fraston Anyitike  amesema kwa kushirikiana na watumishi wa halmashauri kuweza kutoa elimu juu ya  matumizi  ya kifedha  hizo  ili  zilete  tija  kwa kaya  hizo  maskini  kwa kipindi  chote cha  utekelezaji wa mradi.

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.