KILIMO CHA UMWAGILIAJI HATARINI KUTOWEKA CHAMKOLOMA-KISA UHARIBIFU WA MAZINGIRA.



N a Stephen noel – Kongwa.
KILIMO Cha  umwagiliaji  katika   kata ya chamkoloma   wilyani Kogwa  kipo hataririni kutoweka  na kufutika kabisa kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea katika vijiji vya  Tubugwe juu, Mseta,Kiboriani, na kijiji cha Sagala.
Ras fm  imetembelea  maeneo hayo  ambayo ambayo ni    Tubugwe kibaoni, tubugwe juu,mseta A, Mseta bondeni,chamkoloma, makole na ambapo ilijionea uharibifu mkubwa wa mazingira ,ikiwemo wanachi wa  vijiji hivyo   kukata miti sana katika  milima hiyo na kulima katika vyanzo vya maji,  ambayo imekua ni tishio kubwa  kwa baadhi ya mabonde kuanza kukausha maji na kupungua kwa uzalishaji  wa mazao kama miwa na maharage  yanayo limwa  katika mabonde hayo.
Mtendaji  kata  ya chamkolama  Bwana Fanuel Ng’anda alisema kata hiyo  ambayo imekuwa ni tegemeo kubwa la mazao ya mbogamboga  ambayo hulisha karibu mkoa mzima wa Dodoma  na mkoa jirani kama  morogoro ambayo alisema kwa sasa imepungua sana.
Aidha alisema siku  hadi siku zinavyo zidi kusonga mbele tatizo linazidi kuwa  kubwa  na maji yanazidi kupungua na kutishia kukauka kwa vyanzo vya maji  ambavyo ndivo tegemeo kubwa la maisha ya watu wa kata hiyo.
 Hatahivyo  alisema   kuna baadhi ya wanasiasa wamekuwa kikwazo katika  kulifanikisha suala hilo ambalo alisema ni kuwakingia vifua waharibifu wa mazingira kwa madai ya kupoteza kura hasa katika kipindi hiki cha kuelekea  katika kipindi cha uchaguzi October mwaka huu.
Kwa upande wake  A mos Leganga  mwenyekiti wa  mradi wa maji  mesema kuwa kutokana na  shughuli  kubwa za kibinadamu kufanyika katika milima ya hifadhi, kulima katika vyanzo ya maji  kunatishia uendelevu wa upatikanaji wa nmaji safi katika vijiji hivyo.
Pia alisema kumekuwako na changamoto kubwa ya viongozi wa  wilaya ya mpwapwa na wilaya ya kongwa kushidwa kuafikiana  juu ya mbinu zitakazo nusuru mlima wa kiboriani  ambao ndio chazo kikubwa cha upatikanaji wa , maji katika wilaya hizo  kwa sababu alizo ziita kuwa ni za wanasiasa kuwalinda waharibifu wa mazingira.
Hata hivyo alisema milima hiyo imeanza kuonyesha  uhafadhali baada ya kukabidhiwa kwa wakala wa misitu  kusimamia,  tofauti na hapo awali ambapo milima hiyo ilikuwa inasimamiwa na serikali za vijiji ambazo zimeonyesha  kushidwa kutatua tatizo hilo.
Diwani wa kata ya chamkoloma  Daimon Mdumbe  alikanusha kwa baadhi yawanasiasa wakiwemo madiwani kuhusika katika kuwakingia vifua waharibifu wa mazingira kwa kile alicho kisema kuwa,  maisha ni zaidi ya kura wanazo zipata  hivyo aliwataka  watendaji wote wa serikali kufuata sheria na taratibu za kazi  kuwaadhibu waharifu  wa mazingira.
Aliongeza kuwa milima wa Kiboriani  ambao ndio mlima mkubwa ambao upo katika hifadhi za milima za tao  ya mashariki lakini umehribiwa sana  kitu alicho kisema kuwa wamepanga kukaa kikao cha pamoja  na uongozi wa wilaya ya mpwapwa pamoja na kongwa ili kuweza kutafuta njia ya pamoja ya kulitatua tatizo hilo.
Ikumbukwe kuwa katika katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 katika sehemu ya tatu  juu yahaki na wajibu kifungu cha 27 kinachodai kila mtu  ana haki ya kulinda mali asilia sambamba na sheria ya kulinda mali ya umma  ya mwaka 1984 namba 5 ibara 6 hivyo anaye haribu mazingira anakinzana na katiba hii.


Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.